´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kulala akakosa sehemu yake ya usiku au sehemu yake, kisha akaisoma kati ya swalah ya Fajr na swalah ya Dhuhr, basi ataandikiwa kama kwamba aliisoma usiku.”[1]
Ameipokea Muslim.
Sulaymaan bin Yasaar ameeleza ya kwamba Abu Usayd (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Nililala jana usiku nikakosa sehemu yangu ya kusoma mpaka nikafika asubuhi. Nilipoamka nilisema:
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ
”Hakika sisi ni wa Allaah na hakika Kwake tutarejea.”
Sehemu yangu ilikuwa ni Suurah al-Baqarah. Nikamuona katika ndoto kama kwamba ng’ombe ananipiga kwa pembe.”
Ameipokea Ibn Abiy Daawuud.
Ibn Abiyd-Dunyaa ameeleza:
”Bwana mmoja, ambaye alikuwa amehifadhi Qur-aan, alilala usiku mmoja ambapo akakosa sehemu yake, basi akaoneshwa katika ndoto yake kama kwamba kuna msemaji anayemwambia:
Ninashangaa kwa mwili na afya
na kijana aliyelala mpaka alfajiri
Na kifo hakiaminiki ghafla zake
Katika giza la usiku kinapopita.
[1] Muslim (747), Abu Daawuud (1313), at-Tirmidhiy (581), an-Nasaa’iy (1791-1792) na Ibn Maajah (1343).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 48
- Imechapishwa: 26/08/2026
´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kulala akakosa sehemu yake ya usiku au sehemu yake, kisha akaisoma kati ya swalah ya Fajr na swalah ya Dhuhr, basi ataandikiwa kama kwamba aliisoma usiku.”[1]
Ameipokea Muslim.
Sulaymaan bin Yasaar ameeleza ya kwamba Abu Usayd (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Nililala jana usiku nikakosa sehemu yangu ya kusoma mpaka nikafika asubuhi. Nilipoamka nilisema:
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ
”Hakika sisi ni wa Allaah na hakika Kwake tutarejea.”
Sehemu yangu ilikuwa ni Suurah al-Baqarah. Nikamuona katika ndoto kama kwamba ng’ombe ananipiga kwa pembe.”
Ameipokea Ibn Abiy Daawuud.
Ibn Abiyd-Dunyaa ameeleza:
”Bwana mmoja, ambaye alikuwa amehifadhi Qur-aan, alilala usiku mmoja ambapo akakosa sehemu yake, basi akaoneshwa katika ndoto yake kama kwamba kuna msemaji anayemwambia:
Ninashangaa kwa mwili na afya
na kijana aliyelala mpaka alfajiri
Na kifo hakiaminiki ghafla zake
Katika giza la usiku kinapopita.
[1] Muslim (747), Abu Daawuud (1313), at-Tirmidhiy (581), an-Nasaa’iy (1791-1792) na Ibn Maajah (1343).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 48
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/38-kupitiwa-na-usingizi-na-kukosa-kisomo-cha-usiku/