Imethibiti kutoka kwa Abu Muusaa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Iangalieni hii Qur-aan! Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi Mwake, hakika ni yenye kutoroka zaidi kuliko ngamia walioko katika kamba zao.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa mwenye Qur-aan ni kama mfano wa ngamia waliofungwa; akiwatunza anawashikilia, na akiwaachia wanaondoka.”[2]

Ameipokea Muslim na al-Bukhaariy.

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zilioneshwa kwangu thawabu za ummah wangu, hata uchafu mdogo anaoutoa mtu msikitini, na zilioneshwa kwangu dhambi za ummah wangu, basi sikuona dhambi kubwa zaidi kuliko Suurah katika Qur-aan au Aayah aliyopewa mtu kisha akaisahau.”[3]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy. Hata hivyo imetiwa dosari.

Sa´d bin ´Ubaadah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusoma Qur-aan kisha akaisahau atakutana na Allaah (´Azza wa Jall) siku ya Qiyaamah hali ya kuwa amekatwa mkono.”[4]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy.

[1] al-Bukhaariy (5033) na Muslim (791).

[2] al-Bukhaariy (5031) na Muslim (789).

[3] Abu Daawuud (461) na at-Tirmidhiy (2916). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (461).

[4] Abu Daawuud (1474) na ad-Daarimiy (3340). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1474).

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 45-47
  • Imechapishwa: 26/08/2026