Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kwamba makaburi ndio mapumziko ya mwisho?
Jibu: Ni haramu na haijuzu kusema hivo. Msemo huo unapelekea kwamba kaburi ndio hatua ya mwisho, jambo ambalo linapelekea kupinga Ufufuliwaji. Ni jambo linalotambulika na waislamu wote kwamba kaburi sio hatua ya mwisho. Labda wale ambao hawaamini Siku ya Mwisho ndio husema kuwa kaburi ndio hatua ya mwisho. Kaburi ndio hatua ya mwisho kwao, lakini sio kwa waislamu. Amesema (Ta´ala) amesema:
أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ
“Kumekughafilisheni kushindana kutafuta kwa wingi mpaka [tahamaki] mkayazuru makaburi.”[1]
Inasemekana kwamba bedui mmoja alimsikia mtu akisoma Aayah hiyo ambapo akasema:
“Naapa kwa Allaah kwamba mtembeaji hadumu hapo. Baada ya matembezi kumalizika kuna uhai wa milele.”
Kwa sababu mtembeaji anakuja na kuondoka. Kwa hivyo ni lazima litokee jambo la Ufufuliwaji, jambo ambalo ndio sahihi. Kwa hivyo ni wajibu kuepuka msemo huo. Kaburi sio kituo cha mwisho. Kituo cha mwisho ni ima Pepo au Moto siku ya Qiyaamah.
[1] 102:01-02
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/453)
- Imechapishwa: 22/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kwamba makaburi ndio mapumziko ya mwisho?
Jibu: Ni haramu na haijuzu kusema hivo. Msemo huo unapelekea kwamba kaburi ndio hatua ya mwisho, jambo ambalo linapelekea kupinga Ufufuliwaji. Ni jambo linalotambulika na waislamu wote kwamba kaburi sio hatua ya mwisho. Labda wale ambao hawaamini Siku ya Mwisho ndio husema kuwa kaburi ndio hatua ya mwisho. Kaburi ndio hatua ya mwisho kwao, lakini sio kwa waislamu. Amesema (Ta´ala) amesema:
أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ
“Kumekughafilisheni kushindana kutafuta kwa wingi mpaka [tahamaki] mkayazuru makaburi.”[1]
Inasemekana kwamba bedui mmoja alimsikia mtu akisoma Aayah hiyo ambapo akasema:
“Naapa kwa Allaah kwamba mtembeaji hadumu hapo. Baada ya matembezi kumalizika kuna uhai wa milele.”
Kwa sababu mtembeaji anakuja na kuondoka. Kwa hivyo ni lazima litokee jambo la Ufufuliwaji, jambo ambalo ndio sahihi. Kwa hivyo ni wajibu kuepuka msemo huo. Kaburi sio kituo cha mwisho. Kituo cha mwisho ni ima Pepo au Moto siku ya Qiyaamah.
[1] 102:01-02
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/453)
Imechapishwa: 22/07/2026
https://firqatunnajia.com/389-kaburi-ndio-kituo-cha-mwisho/