Swali: Katika baadhi ya maeneo wana mazowea ya kupanda vichaka na mimea kwenye makaburi au pembezoni mwake kwa namna ya kwamba yule anayeingia kwenye eneo la kuzikia huona vichaka na mimea mingi. Ni ipi hukumu hukumu ya hilo?
Jibu: Makaburini ni mahali wanapozikwa wafu, sio mahali pa kupanda. Lakini pengine watu hawa wanataka kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale alipopita karibu na makaburi mawili na akasema:
Hakika wawili hawa wanaadhibiwa na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Lakini hata hivyo ni jambo kubwa. Kuhusu mmoja wao alikuwa akitembea na kueneza umbea na mwengine alikuwa hajichungi na mkojo wake. Baada ya hapo akachukua kuti na akaligawa mara mbili na akaweka kwenye kila kaburi kuti moja. Wakasema: “Mtume wa Allaah! Kwa nini umefanya hivo?” Akasema: “Pengine wakakhafifishiwa adhabu midhali bado [makuti hayo] ni kijani.”[1]
Ikiwa haya ndio makusudio yao basi wamekosea kwa njia nyingi:
1 – Jambo hilo haikuwa ni katika mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kila kaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya juu ya hayo mawili makaburi kwa sababu alijuzwa ya kwamba wanaadhibiwa. Kwa maana nyingine kufanya hivo juu ya kila kaburi ni Bid´ah na kwenda kinyume na matendo yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kutofanya hivo juu ya kila kaburi.
2 – Kufanya hivo ni kumjengea dhana mbaya yule maiti na kufikiria kwamba anaadhibiwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoa sababu za kufanya hivo na akaweka kuti juu ya makaburi yao. Je, watu hawa wanafikiria kuwa baba, watoto, ndugu na marafiki zao wanaadhibiwa?
3 – Maji haya yanayomwagiliwa makaburi haya yataingia ndani ya kaburi. Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa kaburi lililozungukwa na maji lichimbwe kwa sababu yanamlowanisha yule maiti. Kusemwe nini juu ya ambaye anamwagilia maji makaburi na hivyo maji yakaingia moja kwa moja kule ndani ya kwa maiti? Hivyo ninawashauri waache kufanya hivyo na wajiepushe na wajiondoe khofu wao wenyewe na wafu wao kutokana na taabu hii.
14/03/1418
[1] al-Bukhaariy (218) na Muslim (292).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/449)
- Imechapishwa: 22/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/449)
Imechapishwa: 22/07/2026
https://firqatunnajia.com/384-je-inafaa-kupanda-vichaka-makaburini/