Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujua maana ya zile sifa za Allaah alizoteremshiwa Allaah kupitia Jibriyl (´alayhis-Salaam). Wala Jibriyl na wale wa waliotangulia wa mwanzo hawakujua maana ya Aayah hizo. Vivyo hivyo wanasema kuwa maana ya Hadiyth zinazozungumzia sifa za Allaah hakuna anayezijua isipokuwa Allaah pekee, ingawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianza kuzungumza nazo. Kwa mujibu wa ´Aqiydah yao ni kwamba alizungumza kitu asichojua maana yake.

MAELEZO

Huku ni kumfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa hajui au hafahamu maana ya yale aliyoteremshiwa katika sifa za Allaah. Na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kumwambia:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

“Tumekuteremshia Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao na huenda wakapata kuzingatia.”[1]

Ni vipi atawabainishia watu ilihali yeye mwenyewe hafahamu maana ya Aayah? Vivyo hivyo wamemzulia uongo kwamba anabeba matamshi ya kigeni ambayo hayafahamiki maana yake. Kama walivyosema kuhusu Aayah, ndivyo walivyosema pia juu ya Hadiyth zilizopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu sifa za Allaah; kwamba maana yake haifahamiki. Wamekadhibisha katika hili. Hadiyth zimezungumzwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, anaweza kuzungumza kitu ambacho hafahamu maana yake?

[1] 16:44

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 256
  • Imechapishwa: 22/07/2026