381. Kicheko na mazungumzo ya kidunia makaburini

Swali: Baadhi ya watu wa kawaida wanapofika makaburini wanaanza kuongea porojo na mambo ya kilimwengu. Ni zepi nasaha zako kwa mwenye kuyatembelea makaburi na kusindikiza jeneza? Ajishughulishe na nini?

Jibu: Nasaha zetu kwa ambaye anayatembelea makaburi aombe yale yaliyopokelewa katika Sunnah:

السلام عليكم دار قوم مؤمنين، وإنا إن شاءالله بكم لاحقون، يرحم الله المستقدمين منا ومنكم والمستأخرين، نسأل الله لنا ولكم العافية، اللهم لا تحرمنا أجرهم، ولا تفتنا بعدهم، واغفر لنا ولهم

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Allaah awarehemu wale waliotangulia katika sisi na katika nyinyi na wale wataokuja baadaye. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi uzima. Allaah! Usitunyime ujira wao, usitutahini baada yao na utusamehe sisi na wao.”[1]

Haifai kwa mwenye kuyatembelea kuongea chochote katika mambo ya kilimwengu, kichekesho na mfano wa hayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yatembeleeni makaburini. Kwani hakika yanakukumbusheni Aakhirah.”[2]

Kwa hivyo Sunnah katika kuyatembelea makaburi ni mtu awe mwenye kukumbuka, mnyenyekevu, mwenye kutafuta unyenyekevu, mwenye kukumbuka hatima yake na kwamba siku moja yatamfika yale yaliyofika watu hawa.

[1] Muslim (974).

[2] Muslim (976).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/444-445)
  • Imechapishwa: 20/07/2026