152. Kwanini mnaamini Kufufuliwa kisha mnapinga Sifa?

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Kwa msemo mwingine ni kwamba kukubali kwa akili jambo la sifa za Allaah ni kukubwa zaidi kuliko kukubali kwake jambo la Kufufuliwa na kwamba kupinga sifa za Allaah ni jambo la khatari zaidi kuliko kupinga Kufufuliwa. Ni vipi basi yale aliyoeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu sifa za Allaah isiwe kama yale aliyoeleza kuhusu Kufufuliwa ilihali yale aliyoeleza kuhusu Kufufuliwa yawe kama alivosema?

MAELEZO

Kukubali kwa akili kuhusu sifa za Allaah ni kukubwa zaidi kuliko kukubali kwake kuhusu Kufufuliwa. Hili linathibitisha ubatili wa kauli ya wanaokanusha sifa kwa kutumia akili. Kwa mujibu wa fikira zao ni kwamba kupinga Kufufuliwa ni khatari zaidi kuliko kupinga sifa za Allaah. Ukweli wa mambo ni kwamba kupinga sifa za Allaah ndio khatari zaidi kuliko kupinga Kufufuliwa. Kwa hiyo, ikiwa nyinyi Mu´tazilah, mnaona kuwa yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaeleza kuhusu Kufufuliwa ni haki kwa maana yake ya kweli, basi kwa nini majina na sifa za Allaah zisiwe juu ya maana zake za kweli, hali ya kuwa Maandiko yake ndani ya Qur-aan ni mengi zaidi kuliko Maandiko ya kufufuliwa?

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 250
  • Imechapishwa: 20/07/2026