Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Aidha ni jambo linalojulikana kuwa washirikina wa kiarabu na wengineo walikuwa wakimpinga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu jambo la kuamini Kufufuliwa tofauti na jambo la kuamini sifa za Allaah – hakuna yeyote katika waarabu ambaye alimpinga juu ya jambo hilo.

MAELEZO

Hii ni namna nyingine katika kuwaraddi wale wanaopindisha maana ya sifa za Allaah. Waarabu katika zama kabla ya kuja Uislamu walikuwa wakikanusha Kufufuliwa na kusema:

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ قَالَ تَاللَّـهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ

“Je, tutakapokufa, tukawa udongo na mifupa, eti kweli sisi tutahukumiwa?” Atasema: “Je, mngependa kuchungulia?” – Basi akapitisha macho, akamuona [rafiki yake] yuko katikati moto uwakao vikali mno akasema: “Naapa kwa Allaah! Ulikaribia kuniangamiza; na lau kama si neema ya Mola wangu, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wahudhurishwao! Je, sisi hatutakufa tena? Isipokuwa kifo chetu cha kwanza, nasi hatutaadhibiwa. Hakika huku ndiko kufuzu kukubwa! Kwa mfano wa haya basi watende wenye kutenda!”[1]

Hata hivyo hawakuwa wakikanusha majina na sifa za Allaah. Mayahudi pia hawakuyakanusha majina na sifa. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Rabi mmoja katika mayahudi alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Itapofika siku ya Qiyaamah Allaah ataziweka mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, milima na miti kwenye kidole, maji na udongo kwenye kidole na viumbe wengine wote kwenye kidole. Kisha avitikise na kusema: “Mimi ndiye Mfalme! Mimi ndiye Mfalme!” Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akicheka mpaka magego yake yakaonekana hali ya kustaajabu na kuthibitisha maneno yake. Halafu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[2]

Kwa hiyo yaliyomo ndani ya Qur-aan yamesadikisha yaliyomo ndani ya Tawraat. Hivyo mayahudi hawakanushi majina na sifa. Waarabu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu hawakanushi majina na sifa. Lakini nyinyi mnakanusha majina na sifa. Kwa hiyo nyinyi mpo katika upotofu mkubwa zaidi kuliko mayahudi na watu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu katika maudhui haya.

[1] 37:16-17

[2] 39:67 al-Bukhaariy (4811) na Muslim (2786).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 249-250
  • Imechapishwa: 20/07/2026