Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Katika hali hiyohiyo Ahl-us-Sunnah wanawaambia kuwa tunajua kwa yakini ya kwamba Mitume wamekuja hali ya kuthibitisha maandiko ya sifa. Maandiko kuhusu sifa katika vitabu vya kiungu ni vingi na zaidi kuliko maandiko ya Qiyaamah.
MAELEZO
Ahl-us-Sunnah waliwaambia Mu´tazilah: Ikiwa Kufufuliwa na kuhuishwa ni haki na nyinyi mnawaraddi wanafalsafa wanaosema kwamba Kufufuliwa si hakika, ingawa Qur-aan imelitaja, basi kwa nini nyinyi mnayapindisha maana majina na sifa za Allaah na kusema kwamba si za hakika? Mnadai kuwa ´Aqiydah yao wao ni batili na ´Aqiydah yenu nyinyi ndio sahihi.
Kwa hiyo Ahl-us-Sunnah wanawaraddi makundi yote mawili; wale wanaofuata mawazo na wale wanaopindisha maana. Wanaona kuwa makundi yote mawili ni batili kwa sababu hawakujengea ´Aqiydah yao kutokana na Qur-aan na Sunnah. Dalili yao pekee ni kanuni zao wenyewe. ´Aqiydah zote mbili ni batili. Haki ni yale waliokuwa juu yake Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hivyo ikiwa madhehebu ya wanafalsafa katika kupindisha maana ya Kufufuliwa ni mabovu, basi ubovu wa madhehebu ya wenye kupindisha majina na sifa ni mkubwa zaidi. Maandiko ya sifa katika vitabu vya mbinguni, kama vile Tawraat, Injiyl, Qur-aan na vitabu vingine vilivyoteremshwa, yamejaa zaidi kuliko kutajwa kwa Kufufuliwa, Pepo na Moto. Kwa hiyo kwa nini mnawakalia kooni wale wanaofuata mawazo katika kukanusha Kufufuliwa hali ya kuwa nyinyi wenyewe mnafanya jambo kubwa zaidi na lililotajwa zaidi katika Qur-aan na vitabu vyengine vya mbinguni, nalo ni kupindisha majina na sifa za Allaah?
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 248-249
- Imechapishwa: 20/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Katika hali hiyohiyo Ahl-us-Sunnah wanawaambia kuwa tunajua kwa yakini ya kwamba Mitume wamekuja hali ya kuthibitisha maandiko ya sifa. Maandiko kuhusu sifa katika vitabu vya kiungu ni vingi na zaidi kuliko maandiko ya Qiyaamah.
MAELEZO
Ahl-us-Sunnah waliwaambia Mu´tazilah: Ikiwa Kufufuliwa na kuhuishwa ni haki na nyinyi mnawaraddi wanafalsafa wanaosema kwamba Kufufuliwa si hakika, ingawa Qur-aan imelitaja, basi kwa nini nyinyi mnayapindisha maana majina na sifa za Allaah na kusema kwamba si za hakika? Mnadai kuwa ´Aqiydah yao wao ni batili na ´Aqiydah yenu nyinyi ndio sahihi.
Kwa hiyo Ahl-us-Sunnah wanawaraddi makundi yote mawili; wale wanaofuata mawazo na wale wanaopindisha maana. Wanaona kuwa makundi yote mawili ni batili kwa sababu hawakujengea ´Aqiydah yao kutokana na Qur-aan na Sunnah. Dalili yao pekee ni kanuni zao wenyewe. ´Aqiydah zote mbili ni batili. Haki ni yale waliokuwa juu yake Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hivyo ikiwa madhehebu ya wanafalsafa katika kupindisha maana ya Kufufuliwa ni mabovu, basi ubovu wa madhehebu ya wenye kupindisha majina na sifa ni mkubwa zaidi. Maandiko ya sifa katika vitabu vya mbinguni, kama vile Tawraat, Injiyl, Qur-aan na vitabu vingine vilivyoteremshwa, yamejaa zaidi kuliko kutajwa kwa Kufufuliwa, Pepo na Moto. Kwa hiyo kwa nini mnawakalia kooni wale wanaofuata mawazo katika kukanusha Kufufuliwa hali ya kuwa nyinyi wenyewe mnafanya jambo kubwa zaidi na lililotajwa zaidi katika Qur-aan na vitabu vyengine vya mbinguni, nalo ni kupindisha majina na sifa za Allaah?
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 248-249
Imechapishwa: 20/07/2026
https://firqatunnajia.com/150-sifa-za-allaah-zimetajwa-zaidi-kuliko-qiyaamah/