Swali: Je, adhabu ya kaburi ni miongoni mwa mambo yanayojificha au ni miongoni mwa mambo yenye kushuhudiwa?
Jibu: Adhabu ya kaburi ni miongoni mwa mambo yanayojificha. Ni watu wangapi wanaodhibiwa ndani ya makaburi haya pasi na sisi kuhisi jambo hilo? Ni watu wangapi wanaoneemeshwa kwa kufunguliwa mlango wa Peponi pasi na sisi kuhisi jambo hilo? Hakuna anayejua yaliyoko chini ya makaburi isipokuwa Allaah pekee. Adhabu ya ndani ya kaburi ni miongoni mwa mambo yaliyojificha. Kama isingelikuwa wahy basi tusingelijua chochote juu yake. Wakati alipokuja mwanamke mmoja wa kiyahudi kwa ´Aaishah na akamweleza kuwa maiti huadhibiwa ndani ya kaburi lake, aliogopa mpaka alipokuja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye aliyakubali maneno yake. Lakini Allaah anaweza kumfichukulia amtakaye katika waja Wake. Kama ambavo Alimfichukulia Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu wale mabwana wawili wanaoadhibiwa ambapo mmoja wao alikuwa akieneza umbea na mwingine alikuwa akikojoa hovyo.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/439)
- Imechapishwa: 20/07/2026
Swali: Je, adhabu ya kaburi ni miongoni mwa mambo yanayojificha au ni miongoni mwa mambo yenye kushuhudiwa?
Jibu: Adhabu ya kaburi ni miongoni mwa mambo yanayojificha. Ni watu wangapi wanaodhibiwa ndani ya makaburi haya pasi na sisi kuhisi jambo hilo? Ni watu wangapi wanaoneemeshwa kwa kufunguliwa mlango wa Peponi pasi na sisi kuhisi jambo hilo? Hakuna anayejua yaliyoko chini ya makaburi isipokuwa Allaah pekee. Adhabu ya ndani ya kaburi ni miongoni mwa mambo yaliyojificha. Kama isingelikuwa wahy basi tusingelijua chochote juu yake. Wakati alipokuja mwanamke mmoja wa kiyahudi kwa ´Aaishah na akamweleza kuwa maiti huadhibiwa ndani ya kaburi lake, aliogopa mpaka alipokuja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye aliyakubali maneno yake. Lakini Allaah anaweza kumfichukulia amtakaye katika waja Wake. Kama ambavo Alimfichukulia Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu wale mabwana wawili wanaoadhibiwa ambapo mmoja wao alikuwa akieneza umbea na mwingine alikuwa akikojoa hovyo.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/439)
Imechapishwa: 20/07/2026
https://firqatunnajia.com/adhabu-ya-kaburi-ni-katika-mambo-ya-ghaibu/