Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa mawaidha wakati wa kutoa rambirambi kwa ajili ya kuwakumbusha watu au kutoa mawaidha wakati wa mchakato wa mazishi?
Jibu: Salaf hawakukusanyika kwa lengo la kutoa rambirambi. Kitendo hicho hakikuwekwa katika Shari´ah na kwa ajili hiyo hakuna mikusanyiko wala mawaidha.
Kuhusiana na mawaidha makaburi wakati wa kuzika, ni jambo halikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama akiwakhutubia watu. Kilichopokelewa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika makaburini na kaburi lilikuwa halijachimbwa, akaketi chini na Maswahabah wake wakaketi pembezoni mwake na ndipo akaanza kuwazungumzia yanayomtokea mtu kuanzia pale anapofikwa na kifo mpaka pale anapozikwa. Wakati mwingine ni wakati alipokuwa akimzika mmoja katika wasichana zake akasimama na kuwazungumzisha, lakini sio kwa njia ya khutbah wala mawaidha.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/444)
- Imechapishwa: 23/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa mawaidha wakati wa kutoa rambirambi kwa ajili ya kuwakumbusha watu au kutoa mawaidha wakati wa mchakato wa mazishi?
Jibu: Salaf hawakukusanyika kwa lengo la kutoa rambirambi. Kitendo hicho hakikuwekwa katika Shari´ah na kwa ajili hiyo hakuna mikusanyiko wala mawaidha.
Kuhusiana na mawaidha makaburi wakati wa kuzika, ni jambo halikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama akiwakhutubia watu. Kilichopokelewa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika makaburini na kaburi lilikuwa halijachimbwa, akaketi chini na Maswahabah wake wakaketi pembezoni mwake na ndipo akaanza kuwazungumzia yanayomtokea mtu kuanzia pale anapofikwa na kifo mpaka pale anapozikwa. Wakati mwingine ni wakati alipokuwa akimzika mmoja katika wasichana zake akasimama na kuwazungumzisha, lakini sio kwa njia ya khutbah wala mawaidha.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/444)
Imechapishwa: 23/07/2026
https://firqatunnajia.com/380-ni-ipi-hukumu-ya-kutoa-mawaidha-makaburini/