Swali: Baadhi ya watu wanapoulizwa kuhusu mtu ambaye amekufa punde wanasema: “Allaah amemkumbuka.” Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa anakusudia kuwa Allaah amemkumbuka kisha ndio akachukua uhai wake, haya ni maneno ya kikafiri. Kwa sababu hiyo maana yake ni kwamba Allaah (´Azza wa Jall) anasahau. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hasahau kabisa. Kama alivyosema Muusa (´alayhis-Salaam) kumwambia Fir´awn wakati alipomuuliza:

قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى

“Vipi kuhusu hali ya karne za mwanzo?” Akasema: “Ujuzi wake [kuhusu yaliyopitika] uko kwa Mola wangu [yameandikwa] katika Kitabu; hapotezi Mola wangu na wala hasahau.”[1]

Na ikiwa mtu ni mjinga na hakuna anachokusudia isipokuwa kwamba Allaah amemfisha, basi hiyo sio kufuru. Lakini ni lazima kuacha kusema hivo kwa sababu mtu anapata hisia ya kumtia mapungufu Mola (´Azza wa Jall). Badala ya kusema hivo anaweza kusema kuwa Allaah amemfisha au mfano wa hayo.

[1] 20:51-52

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/453-454)
  • Imechapishwa: 23/07/2026