Ufikiriaji ulioamrishwa hapa ambao Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amebainsha ni kwamba moyo unatakiwa kufikiria elimu mbili ili uweze kufikia elimu ya tatu[1]. Ili linawekwa wazi zaidi kwa mifano: Iwapo muislamu atafikiria ukubwa ukubwa wa viumbe hivi, kama vile mbingu, ardhi, Kursiy na ´Arshi, kisha akafikiria kule kushindwa kwake kuvielewa na kuvizunguka kiujuzi, basi ataweza kufikia ujuzi wa tatu; mosi ukubwa na utukufu wa viumbe vyote hivi, pili akili kushindwa kuelewa sifa Zake na kuzizunguka sifa Zake (Subhaanah). Amesema (Subhaanah):

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖوَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا

”Na sema: “Sifa njema zote ni za Allaah ambaye hakujifanyia mwana na wala hakuwa na mshirika katika ufalme na wala hakuwa dhaifu hata awe [ahitaji] mlinzi; basi mtukuze matukuzo makubwa kabisa!”[2]

Allaah kwa kweli ni mkubwa. Sifa zote njema ni Allaah kwa wingi. Kutakasika kutokana na mapungufu ni kwa Allaah, asubuhi na jioni.

[1] Miftaahu Daar-is-Sa´aadah, uk. 181.

[2] 17:111

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 60
  • Imechapishwa: 03/12/2025