38. Mtu anaweza kukufuru kwa neno moja tu bila ya kujua II

na huenda amelisema na huku akidhani ya kwamba yanamkurubisha kwa Allaah, kama walivyokuwa wakidhani washirikina,

MAELEZO

Anaweza kutamka neno la kufuru na huku akidhani kuwa limemkurubisha. Kama mfano walivyokuwa wakisema washirikina:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.” (39:03)

هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

  • Mhusika: maam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 54
  • Imechapishwa: 30/11/2016