Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Kwa sababu vinginevyo hiyo ingelileta maana kwamba hawakujua wala hawakuamini au kwamba waliamini kimakosa. Yote mawili ni mambo yasiyowezekana.

Jambo la kwanza haliwezekani kwa sababu kila mmoja ambaye moyoni mwake mna uhai mdogo, elimu au kivutio cha ´ibaadah anaamini kwamba kuwa na ujuzi juu ya ´Aqiydah ambayo mtu anapaswa kuiamini na kuijua haki kuhusu jambo hilo ndio jambo likubwa ambalo mtu anaweza kujichumia. Hapa sizungumzii ujuzi kuhusu majina ya Allaah na uhakika wa sifa Zake.

MAELEZO

Kusema Mswahabah na wanafunzi wao hawakujua kunaleta maana mbili:

1 – Walikuwa wajinga. Ukweli wa mambo ni kwamba walikuwa ndio wajuzi zaidi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Walificha. Kwa maana nyingine walijua lakini hawakubainisha na wala hawakuwafikishia ujumbe watu. Yote haya mawili wanatakaswa nayo vizazi hivi bora.

Haiwezekani eti walikuwa wajinga juu ya suala hili. Haiwezekani vilevile wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah – ambao ndio walikuwa wajuzi zaidi baada ya Maswahabah – hawakujifunza ´Aqiydah sahihi juu ya Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba walipuuzilia mbali sauala hili. Maudhui haya ndio asili na msingi. Wajishughulishe na elimu nyenginezo? Hili ni jambo lisilowezekana juu yao. Vilevile ni jambo lisilowezekana eti wakawa wameificha elimu hii, kwa sababu hiyo maana yake ni kuwaghushi ummah na ile elimu ambayo walipaswa kuifikisha. Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hapa sizungumzii ujuzi kuhusu majina ya Allaah na uhakika wa sifa Zake.”

Kutambua namna alivyo Allaah na namna zilivyo sifa Zake ni jambo lisilowezekana kwetu. Bali haiwezekani kwetu hata kujua namna na uhakika wa sifa za viumbe wote. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[1]

[1] 20:110

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 05/08/2024