21 – Kuondoa nywele za nyusi

Miongoni mwa makosa yanayopingana na Shari´ah ni kuondoa nywele za nyusi au sehemu yake kwa njia yoyote ile, kwani kufanya hivo ndio Nams ambayo imekatazwa vikali. Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Allaah amewalaani wanawake wanaochora alama kwenye ngozi zao na wanaoomba kuchorwa, wanaonyoa nyusi zao na wanaotia mwanya kwenye meno kwa ajili ya mapambo wanaobadilisha maumbile ya Allaah.” Mwanamke mmoja akamuuliza kuhusu hilo ambapo akajibu: “Kwa nini nisimlaani yule ambaye amelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa ndani ya Kitabu cha Allaah amesema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile anachokupeni Mtume, basi kichukueni, na kile anachokukatazeni, basi kiacheni.”[1]

Hili linazingatiwa kuwa ni kubadilisha maumbile ya Allaah. Kwa hivyo mche Allaah, ee mjakazi wa Allaah, wala usijitie ndani ya laana za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala usibadilishe maumbile ya Allaah.

[1] 59:7

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 19/03/2026