Ahl-ul-Hadiyth wanashuhudia na kuitakidi kuwa mwisho wa matendo ya waja haujulikani. Hakuna yeyote anayejua atamaliza akiwa na hali gani. Hawamuhukumu yeyote kwa dhati kuwa ni katika watu wa Peponi au ni katika watu wa Motoni. Kwa sababu hayo yamefichwa kwao. Hawajui mtu atakufa akiwa na hali gani. Kwa ajili hiyo ndio maana wanasema: Sisi ni waumini – Allaah akitaka.

Wanashuhudia kuwa mafikio ya mwisho ya waislamu ni Peponi. Wale ambao Allaah amekwishatangulia kuamua wataadhibiwa ndani ya Moto kwa kipindi fulani kutokana na madhambi yao waliyofanya pasi na kutubia kwayo, lakini wataingia mwishowe Peponi. Kutokana na fadhilah na neema ya Allaah hakuna muislamu yeyote atakayebaki Motoni. Yule ambaye atakufa juu ya ukafiri ataingia Motoni; hatookolewa humo na wala kubaki kwake kamwe hakuna mwisho. Allaah atulinde!

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 286-287
  • Imechapishwa: 24/12/2023