Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba Allaah ameyataka matendo yote ya waja, ni mamoja matendo yake ya kheri na matendo yake ya shari. Hakuna mtu yeyote aliyeamini isipokuwa kwa matakwa Yake na hakuna yeyote aliyekufuru isipokuwa kwa utashi Wake. Iwapo angelitaka basi angeliwafanya watu wote kuwa ummah mmoja. Angelitaka asiasiwe basi asingemuumba Ibliys. Kukufuru kwa makafiri na kuamini kwa waumini ni kwa mipango, makadirio, matakwa na utashi Wake. Ameyataka yote hayo na kuyakadiria. Anaridhika kwa imani na utiifu na anakasirishwa kwa kufuru na maasi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ

“Mkikufuru, basi hakika Allaah ni mkwasi kwenu, na wala haridhii kwa waja Wake ukafiri.”[1]

[1] 39:7

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 285-286
  • Imechapishwa: 20/12/2023