Abu Yahyaa Zakariyyaa as-Saajiy amesema: al-Muzaniy ametuhadithia:
“Nilijiambia kwamba kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angenikomboa kutokana na swali la upwekeshaji nililokuwa nalo, basi angelikuwa ni ash-Shaafi’iy. Nilimwendea. Alikuwa katika msikiti wa Misri. Nilipiga magoti mbele yake na kusema: “Nimejiliwa akilini mwangu na swali la upwekeshaji na nikajua hakuna yeyote mwenye elimu kama yako. Una la kusema?” Akakasirika na kusema: “Je, unajua wewe ni nani?” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Hapa ndipo pahali Allaah alipomzamisha Fir´awn. Je, umepata khabari kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuuliza juu yake?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: ”Je, Maswahabah wamelilizungumzia?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: ”Je, unajua mbinguni kuna nyota ngapi?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Je, unajua aina ya sayari, machomo na mazamo yake?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: ”Kitu unachokiona kwa macho yako katika viumbe hukukitambua na mnataka kuzungumzia juu ya Muumba wake?” Kisha akaniuliza swali linalohusiana na wudhuu´ ambalo nililijibu kimakosa. Akaligawanya swali hilo katika mafungu manne na sikupatia katika chochote katika hayo. Akasema: “Unapuuza kujua jambo ambalo unalihitaji kwa siku mara tano na unajikakama kumtambua Muumba. Unapoingiwa akilini mwako na kitu katika hayo basi rejea kwa Alllaah na katika maneno Yake (Ta´ala):
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
”Mungu wenu ni Mmoja pekee; hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana na merikebu zipitazo katika bahari kwa vile viwafaavyo watu na maji ambayo Allaah ameyateremsha toka mbinguni akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake na akaeneza humo kila aina ya mnyama na mgeuko wa upepo wa rehema na mawingu yanayotiishwa kati ya mbingu na ardhi ni alama kwa watu wenye akili.”[1]
Ametumia dalili ya kiumbe katika kumthibitisha Muumba. Wala usijikalifishe kuyatambua mambo ambayo hayafikiwi na akili yako.” Nikasema: ”Nikatubia.”[2]
[1] 2:1963-164
[2] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (10/31-32).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 55-56
- Imechapishwa: 03/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 55-56
Imechapishwa: 03/12/2025
https://firqatunnajia.com/36-umeshindwa-kujua-kuhusu-kutia-wudhuu-kisha-unamzungumzia-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket