159 – Abu Nu´aym Ahmad bin ´Abdillaah al-Haafidhw alituhadithia kwa njia ya kututaka tuandike: Muhammad bin Ibraahiym bin al-Muqri’ ametuhadithia: Abu ´Aliy – yaani Ahmad bin ´Aliy bin al-Muthannaa al-Mawsiliy – ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Awn ametuhadithia: ´Uthmaan bin Matwar ash-Shaybaaniy ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit bin al-Bunaaniy, kutoka kwa Mutwarrif bin ´Abdillaah ash-Shikhkhiyr, ambaye amesema:

”Enyi ndugu, jitahidini katika kufanya matendo! Mambo yakiwa kama tunavyotaraji katika rehema na msamaha wa Allaah, basi tutapata daraja Peponi. Na mambo yakiwa mazito kama tunavyoogopa na kujihadhari, basi hatusemi:

رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ

”Ee Mola wetu! Tutoe tufanye mema mbali na ya yale tuliokuwa tukiyafanya!”[1]

Badala yake tunasema ´Tumefanya matendo na hayakutufaa kitu´.”

160 – Abul-Husayn ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Mu-addil ametukhabarisha: Abu ´Aliy al-Husayn bin Swafwaan al-Bardha´iy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-Majiyd amenihadithia: Nimemsikia Sufyaan akisema:

”Mtu mmoja alimwambia Muhammad bin al-Munkadir na bwana mwingine kutoka katika Quraysh: ”Kuweni makini kwelikweli na shikeni tahadhari kwelikweli! Mambo yakiwa kama mnavyotaraji, basi yale yote mliyofanya yatakuwa ni fadhilah. Na mambo yakiwa kinyume na hivyo basi hamtozidhulumu nafsi zenu.”

161 – Abu ´Abdillaah al-Husayn bin ´Umar bin Burhaan al-Ghazzaal ametukhabarisha: ´Abdul-Baaqiy´ bin Qaani´ bin Marzuuq al-Qaadhwiy alituhadithia kwa kututaka tuandike: Bishr bin Muusa ametuhadithia: ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia: Yahyaa bin Humayd bin ´Abdil-Malik bin Abiy Ghaniyyah ametuhadithia: Muhammad bin Naswr al-Haarithiy alimwandikia mmoja katika ndugu zake:

”Hakika hivi sasa unaishi katika maisha ya utangulizi. Mbele yako una makazi mawili ambayo ni lazima uishi moja wapo. Hadi sasa hujadhaminiwa salama ili ufarijike na wala ukanaji ili ufanye mapungufu! Amani iwe nawe!”

[1] 35:37

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 93-94
  • Imechapishwa: 22/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy