245 – ´Aliy bin Muslim amenihadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Hariyz bin ´Uthmaan ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin Maysarah ametuhadithia, kutoka kwa Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa Busr bin Jahhaash al-Qurashiy, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku moja alitema mate kwenye kiganja chake, kisha akaweka kidole chake juu yake na akasema: ”Allaah (´Azza wa Jall) anasema: ”Ee mwana wa Aadam, vipi utashindwa kunishinda hali nimekuumba kutokana na mfano wa hii? Mpaka nilipokukamilisha na nikakusawazisha, ukatembea huku umevaa vipande viwili vya nguo na kuifanya ardhi kutoa sauti. Unakusanya na unafanya ubakhili. Mpaka ulipofika wakati wa kukata pumzi ya mwisho, ndipo ukasema kuwa unataka kutoa swadaqah. Ni sasa wakati wa kutoa swadaqah?”[1]
246 – Abu Kurayb al-Hamadaaniy ametuhadithia: al-Muhaaribiy ametuhadithia, kutoka kwa Jamiyl bin Zayd, aliyesema:
”Ibn ´Umar alimuona mtu anaburuta kikoi chake akasema mara mbili au mara tatu: ”Hakika shaytwaan anao ndugu zake.”
247 – Ibraahiym bin Sa´iyd ametuhadithia: Muusa bin Ayyuub ametuhadithia: Baqiyyah ametuhadithia, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, ambaye amesema:
”Jiepusheni na mwendo wa majivuno! Kwani mtu anaweza moyo wake ukaenda kinyume na sehemu nyingine ya mwili wake.”
248 – Ibn ´Amr bin Abaan al-Qurashiy ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia:
”Haikuonekana ´Aliy bin Husayn akitembea akipiga mikono yake namna hii kwa majivuno.”
249 – Khalaf bin Hishaam ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa Yuhannas, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ummah wangu wakitembea kwa maringo na wakatumikishwa na wafursi na warumi, baadhi watawasaliti baadhi ya wengine.”[2]
´Abdullaah amesema:
”Nimemsikia Ibn-ul-A´raabiy akisema kwamba mwendo maringo ni mwendo wa kiburi.”
250 – Ahmad bin Maniy´ ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa Rishdayn bin Kurayb, kutoka kwa baba yake: Nimemsikia al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib akisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mtu alikuja akiwa katika nguo zake mbili akijivuna ndani yake huku akitazama mabegani mwake, basi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) akaamrisha ardhi ikammeza. Anaendelea kuporomoka humo mpaka siku ya Qiyaamah.”
251 – Ahmad bin Yaziyd al-Yaamiy´ ametuhadithia: Husayn bin ´Aliy´ ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiy Rawwaad, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nguo kuteremka chini ya kongo mbili inakuwa katika vitu vitatu: kikoi, kanzu na kilemba.”[3]
[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (2205).
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (801).
[3] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4094).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 290-295
- Imechapishwa: 30/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 290-295
Imechapishwa: 30/03/2026
https://firqatunnajia.com/36-nguo-chini-ya-macho-mawili-ya-miguu-na-kutembea-kwa-maringo/