36. Mtu akivua soksi zake za ngozi baada ya kupangusa juu yake twahara yake inachenguka?

Swali 36: Mtu akivua soksi zake za ngozi baada ya kupangusa juu yake twahara yake inachenguka?

Jibu: Akivua soksi zake za ngozi au soksi za kawaida baada ya kufuta juu yake, twahara yake haichenguki. Haya ndio maoni sahihi. Kinachochenguka ni kule kuendelea kupangusa. Anapoirudisha kwa mara nyingine na ukachenguka wudhuu´ wake basi ni lazima avue soksi zake na aoshe miguu yake.

Muhimu ni kutambua kwamba ni lazima avae soksi za ngozi mtu akiwa na twahara na awe ameosha miguu yake. Kwa sababu mtu huyu wakati alipopangusa juu ya soksi zake za ngozi twahara yake imekamilika kwa mujibu wa dalili ya ki-Shari´ah. Kitu kilichothbiti kwa mujibu wa dalili ya ki-Shari´ah hakichenguki isipokuwa kwa dalili ya ki-Shari´ah. Kujengea juu ya haya wudhuu´ wake hauchenguki pindi anapovua soksi zake za ngozi. Twahara yake bado ni yenye kuendelea mpaka kupatikane moja katika vile vichunguzi vya wudhuu´ vinavotambulika. Lakini, kutokana na ninavojua katika maneno ya wanazuoni, ikiwa baadaye atarejesha soksi zake za ngozi na akataka kupangusa juu yake, haitofaa kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/179)
  • Imechapishwa: 06/05/2021