Swali 36: Je, kuna tofauti kati ya masuala yanayoweza kufichika kwa kawaida na yale yasiyoweza kufichika kama masuala ya Tawhiyd?
Jibu: Ndio, ujinga ambao mtu anaweza kupewa udhuru kwao si katika yale yaliyo wazi. Mjinga ambaye anaweza kupewa udhuru ni katika yale mambo yanayoweza kufichika kwa mtu wa mfano wake. Kwa mfano ikiwa mtu anaishi kati ya waislamu kisha akafanya zinaa na wakati akataka kuadhibiwa akasema kuwa ni mjinga, hatasamehewa kwa sababu jambo hili ni jambo liko wazi. Mfano wa pili akala ribaa ilihali anaishi kati ya waislamu, hatasamehewa. Mfano mwingine akaabudu sanamu ilihali anaishi kati ya waislamu katika jamii ya Tawhiyd, pia hatasamehewa kwa sababu jambo hili ni wazi. Lakini ikiwa kafiri atasilimu katika jamii inayokula ribaa na anawaona watu wakifanya hivyo, kisha naye akala ribaa na akasema kuwa alikuwa mjinga, basi mjinga wa aina hii anaweza kupewa udhuru kwa sababu hajui. Vilevile ikiwa mtu alizaliwa na kukulia katika nchi za mbali na hakuwahi kusikia kuhusu Uislamu na hana njia yoyote ya kufikia elimu, basi mtu wa aina hiyo anapewa udhuru. Hata hivyo mtu anayefanya jambo linalojulikana waziwazi na anaishi kati ya waislamu si mwenye kupewa udhuru. Kwa hiyo masuala yanayoweza kupewa udhuru kwayo lazima yawe magumu, yaliyo mazito na yanayoweza kufichika kwa mtu wa mfano wake. Mfano wa jambo linaloweza kufichika umethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kuhusu yule bwana aliyeamrisha familia yake wamchome moto na pindi alipokaribia kufa aliwakusanya wanawe na kuwauliza
“Nilikuwa baba wa aina gani kwenu?” Wakamsema vizuri. Akawaambia kwamba hakuwahi kufanya jambo lolote jema maishani mwake na kwamba ikiwa Allaah atamfufua, basi atamuadhibu adhabu kali. Akawaagiza watoto wake wamchome moto baada ya kufa, kisha wamponde na kupeperusha majivu yake baharini.”
Imekuja katika mapokezi mengine:
”… tawanyeni nusu ya majivu nchikavu na nusu yake nyingine baharini.”
Watoto wake wakatekeleza maagizo. Kuna Hadiyth nyingine inayosema kwamba Allaah aliziamuru nchikavu na bahari zikusanye kila chembe ya mwili wake, kisha Allaah akamfufua. Allaah akamuuliza: “Ni nini kilichokusukuma kufanya hivyo?” Akajibu: “Kwa sababu ya kukuogop, ee Mola.” Allaah akamrehemu.
Hadiyth hii imejadiliwa na wanazuoni. Baadhi wanasema kwamba hilo linahusu Shari´ah za waliokuwa kabla yetu. Lakini maoni sahihi zaidi ni yale aliyoeleza Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
”Mtu huyu alifanya hivyo kwa sababu ya ujinga. Alidhani kwamba angeweza kumponyoka Allaah kama mwili wake ungeharibiwa kabisa. Kwa hivyo hakuwa anakana ufufuo wala uwezo wa Allaah. Bali alikosea katika kuelewa ukamilifu wa uwezo wa Allaah kwa kufikiri kwamba ikiwa mwili wake ungechomwa na kuharibiwa, hangeweza kufufuliwa. Kilichompelekea kufanya hivo ni khofu yake kubwa, si ukaidi wala ukanushaji. Ndipo Allaah akamsamehe. Kama angekuwa mjuzi na bado akafanya hivyo, asingesamehewa. Vivyo hivyo kama angekuwa mkaidi, asingesamehewa. Hata hivyo hakuwa mkaidi wala mjuzi na hivyo akakusanyikiwa na ujinga na khofu kubwa. Matokeo yake Allaah akamsamehe na kumrehemu. Hili ni mfano wa mambo ambayo ni yenye kujificha na nyeti juu ya mtu huyu.
Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah wake wote.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 74-76
- Imechapishwa: 09/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 74-76
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/36-je-kuna-tofauti-kati-ya-masuala-yanayoweza-kufichika-kwa-kawaida-na-yale-yasiyoweza-kufichika-kama-masuala-ya-tawhiyd/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket