29. Dalili ya ishirini na saba kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

27- Muhammad ametukhabarisha: Ahmad bin al-Hasan ametuhadithia: Abul-Qaasim ´Abdur-Rahmaan bin ´Ubaydillaah al-Hirfiy ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Sulaymaan an-Najjaad ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah bin Sulaymaan ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Bakr ametuhadithia: Zaa-idah bin Abiyr-Raqaad ametuhadithia, kutoka kwa Ziyaad an-Numayriy, kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh), kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Niliingia kwa Mola wangu (´Azza wa Jall) wakati alipokuwa juu ya ´Arshi Yake (Tabaarak wa Ta´ala).”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Zaa-idah ni dhaifu. Matini ya Hadiyth imepokelewa katika ”as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia kwa Qataadah, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

”Nilimuomba Mola wangu idhini ya kuingia Kwake, ambapo nikapewa.”

Ameipokea Abu Ahmad al-´Assaal katika ”Kitaab-ul-Ma´rifah” kwa cheni ya wapokezi yenye nguvu kupitia kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambapo imekuja:

”Nikafika kwenye mlango wa Pepo ambapo nikafunguliwa. Nikafika kwa Mola wangu na Alikuwa kwenye Kursiy Yake ambapo nikashuka chini kwa kusujudu.” (al-´Uluww, uk. 32)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 111
  • Imechapishwa: 08/06/2018