28. Dalili ya ishirini na sita kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

26- Twaahir bin Muhammad al-Maqdisiy ametukhabarisha: Abul-Hasan Makkiy bin Mansuur ametuhadithia: Abu Bakr al-Jarshiy ametuhadithia: Abul-´Abbaas al-Asamm ametuhadithia: ash-Shaafi´iy ametuhadithia: Ibraahiym bin Muhammad amenihadithia: Muusa bin ´Ubaydah amenihadithia: Abul-Azhar Mu´aawiyah bin Ishaaq bin Twalhah amenihadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umayr ambaye ameeleza kwamba alimsikia Anas bin Maalik akisema:

“Jibriyl (´alayhis-Salaam) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na kio cheupe kilicho na madoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ni kitu gani hichi?” Akasema: “Hii ni ijumaa. Wewe na Ummah wako mmefadhilishwa kwayo. Watu, mayahudi na manaswara, watakuwa ni wenye kuwafuata. Ni yenye kheri kwenu. Ndani yamo kuna saa/wakati ambao hakuna mja yeyote muumini ambaye atamuomba Allaah kitu cha kheri isipokuwa atamuitikia. Siku hiyo kwetu ni siku yenye kuzidi.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Jibriyl! Ni nini siku yenye kuzidi.”Akasema: “Mola wako ameumba bonde Peponi. Ndani yake mna mchanga wa miski. Inapokuwa siku ya ijumaa Allaah (´Azza wa Jall) anawashusha Malaika anaowataka. Pembezoni Mwake kuna mimbari za nuru. Juu yake ndiko kuna nafasi za Mitume. Mimbari hizo zitazungukwa na mimbari za dhahabu, zimepambwa kwa yakuti. Humo watakuwa mashahidi na wakweli ambao watakaa nyuma ya mchanga huo. Allaah atawaambia: “Mimi ndiye Mola wenu. Nimekutekelezeeni ahadi Yangu. Niulizeni Nikupeni.” Waseme: “Ee Mola wetu! Tunakuomba radhi Zako.” Aseme: “Nimekuridhieni. Nitakupeni kile mnachokitamani na mimi Kwangu kuna ziada.”Wataipenda siku ya ijumaa kutokana na ile kheri ambayo Mola wao amewapa ndani yake. Hiyo ndio siku ambayo Mola wenu alilingana juu ya ´Arshi, kaumbwa Aadam na ndio siku itasimama Saa.”[1]

[1] ash-Shaafi´iy katika ”al-Musnad” (374). adh-Dhahabiy amesema:

”Ibraahiym na Muusaa ni madhaifu.” (al-´Uluww, uk. 30)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 08/06/2018