Inampasa awe na uangalizi mkubwa zaidi katika kusoma Qur-aan usiku. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ
”Hawalingani sawasawa; miongoni mwa Watu wa Kitabu wako watu wenye kusimama wanazisoma Aayah za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu. Wanamwamini Allaah na siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na kukemea maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri – na hao ni miongoni mwa waja wema.”[1]
Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ni mtu mwema ´Abdullaah lau angekuwa anaswali usiku.”[2]
Imesihi katika Hadiyth nyingine ya kuwa amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ee ´Abdullaah! Usiwe kama fulani; alikuwa anasimama usiku kisha akaacha.”[3]
Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Utukufu wa muumini ni kusimama usiku.”[4]
Ameipokea at-Twabaraaniy na wengineo. Kuna Hadiyth na masimulizi mengi mfano wa hayo.
Abul-Ahwasw al-Habashiy amesema:
”Hakika mtu alikuwa anakuja kwenye hema usiku, basi anasikia kwa watu wake sauti kama mvumo wa nyuki, akasema: ”Imekuwaje hawa wanajiamini na kile ambacho wale walikuwa wanakiogopa?”
Ibraahiym an-Nakha´iy amesema:
”Someni usiku hata kama ni muda wa kukamua kondoo.”
Yaziyd ar-Riqaashiy amesema:
”Nikilala, kisha nikaamka, kisha nikalala, basi macho yangu yasipate usingizi.”
[1] 3:113-114
[2] al-Bukhaariy (3740) na Muslim (2478).
[3] al-Bukhaariy (1152) na Muslim (1159).
[4] at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” (4278). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (73).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 43
- Imechapishwa: 26/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 43
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/35-usomaji-wa-qur-aan-usiku/