Ama kuhusu wakati wa kuanza na kumaliza kwa yule anayeikhitimisha katika wiki, Ibn Abiy Daawuud amepokea kwamba ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa anaanza kuisoma Qur-aan usiku wa ijumaa na kuimaliza usiku wa alkhamisi. Imaam Abu Haamid al-Ghazaaliy (Rahimahu Allaah) amesema katika ”al-Ihyaa”:
”Lililo bora ni kuisoma yote mara moja usiku na nyingine mchana; afanye hitimisho moja ya mchana siku ya jumatatu katika Rak´ah mbili za Fajr au baada yake, na afanye hitimisho nyingine usiku wa ijumaa katika Rak´ah mbili za Maghrib au baada yake, ili aupokee mwanzo wa mchana na mwisho wake.”
Ibn Abiy Daawuud amepokea kutoka kwa mwanafunzi wa Maswahabah ´Umar bin Murrah, ambaye amesema:
”Walikuwa wanapenda kuisoma Qur-aan yote mwanzoni mwa usiku au mwanzoni mwa mchana.”
Mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah Twalhah bin Muswarrif amesema:
”Mwenye kuisoma Qur-aan yote wakati wowote wa mchana, basi Malaika humswalia mpaka jioni. Na wakati wowote wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kupambazuke asubuhi.”
Mujaahid amesema mfano wa hayo. ad-Daarimiy amepokea kwamba Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Ikiwa usomaji wote wa Qur-aan utakutana na mwanzo wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kupambazuke asubuhi. Na ikiwa utakutana na mwisho wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kuingie jioni.”[1]
ad-Daarimiy amesema:
”Hii ni nzuri kutoka kwa Sa´d.”
Mwanafunzi wa Maswahabah Habiyb bin Abiy Thaabit alikuwa akiisoma Qur-aan yote kabla ya kwenda katika Rukuu´. Ibn Abiy Daawuud amesema:
”Vivyo hivyo amesema Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah).”
Sehemu nyingine ya mlango huu itayokuja huko mbele – Allaah akitaka.
[1] ad-Daarimiy (3482).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 42
- Imechapishwa: 26/08/2026
Ama kuhusu wakati wa kuanza na kumaliza kwa yule anayeikhitimisha katika wiki, Ibn Abiy Daawuud amepokea kwamba ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa anaanza kuisoma Qur-aan usiku wa ijumaa na kuimaliza usiku wa alkhamisi. Imaam Abu Haamid al-Ghazaaliy (Rahimahu Allaah) amesema katika ”al-Ihyaa”:
”Lililo bora ni kuisoma yote mara moja usiku na nyingine mchana; afanye hitimisho moja ya mchana siku ya jumatatu katika Rak´ah mbili za Fajr au baada yake, na afanye hitimisho nyingine usiku wa ijumaa katika Rak´ah mbili za Maghrib au baada yake, ili aupokee mwanzo wa mchana na mwisho wake.”
Ibn Abiy Daawuud amepokea kutoka kwa mwanafunzi wa Maswahabah ´Umar bin Murrah, ambaye amesema:
”Walikuwa wanapenda kuisoma Qur-aan yote mwanzoni mwa usiku au mwanzoni mwa mchana.”
Mwanafunzi mtukufu wa Maswahabah Twalhah bin Muswarrif amesema:
”Mwenye kuisoma Qur-aan yote wakati wowote wa mchana, basi Malaika humswalia mpaka jioni. Na wakati wowote wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kupambazuke asubuhi.”
Mujaahid amesema mfano wa hayo. ad-Daarimiy amepokea kwamba Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Ikiwa usomaji wote wa Qur-aan utakutana na mwanzo wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kupambazuke asubuhi. Na ikiwa utakutana na mwisho wa usiku, basi Malaika humswalia mpaka kuingie jioni.”[1]
ad-Daarimiy amesema:
”Hii ni nzuri kutoka kwa Sa´d.”
Mwanafunzi wa Maswahabah Habiyb bin Abiy Thaabit alikuwa akiisoma Qur-aan yote kabla ya kwenda katika Rukuu´. Ibn Abiy Daawuud amesema:
”Vivyo hivyo amesema Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah).”
Sehemu nyingine ya mlango huu itayokuja huko mbele – Allaah akitaka.
[1] ad-Daarimiy (3482).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 42
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/34-muda-ambao-qur-aan-inasomwa-yote/