Lililo bora ni kwamba hilo hutofautiana kwa watu. Mwenye kufungukiwa na ufahamu wa ndani na maarifa ya kina, basi ajitosheleze na kiasi kinachomwezesha kupata ufahamu kamili wa anachokisoma. Vilevile yule mwenye kushughulishwa na kusambaza elimu au mambo mengine muhimu ya dini na maslahi ya waislamu kwa ujumla, basi ajitosheleze na kiasi ambacho hakitasababisha upungufu katika alichowekewa jukumu. Ikiwa si miongoni mwa hao waliotajwa, basi azidishe kadiri awezavyo bila kufikia kiwango cha kuchoka au kusoma kwa haraka bila mpangilio.
Baadhi ya waliotangulia wamechukia kuisoma Qur-aan yote katika mchana mmoja na usiku wake. Jambo hili linaungwa mkono na Hadiyth Swahiyh kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Haifahamu Qur-aan yule anayesoma chini ya siku tatu.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh, an-Nasaa´iy na wengineo – Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] Abu Daawuud (1394), at-Tirmidhiy (2949), ambaye amesema kuwa ni nzuri na Swahiyh, Ibn Maajah (1347). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (1394).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 41
- Imechapishwa: 26/08/2026
Lililo bora ni kwamba hilo hutofautiana kwa watu. Mwenye kufungukiwa na ufahamu wa ndani na maarifa ya kina, basi ajitosheleze na kiasi kinachomwezesha kupata ufahamu kamili wa anachokisoma. Vilevile yule mwenye kushughulishwa na kusambaza elimu au mambo mengine muhimu ya dini na maslahi ya waislamu kwa ujumla, basi ajitosheleze na kiasi ambacho hakitasababisha upungufu katika alichowekewa jukumu. Ikiwa si miongoni mwa hao waliotajwa, basi azidishe kadiri awezavyo bila kufikia kiwango cha kuchoka au kusoma kwa haraka bila mpangilio.
Baadhi ya waliotangulia wamechukia kuisoma Qur-aan yote katika mchana mmoja na usiku wake. Jambo hili linaungwa mkono na Hadiyth Swahiyh kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Haifahamu Qur-aan yule anayesoma chini ya siku tatu.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh, an-Nasaa´iy na wengineo – Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] Abu Daawuud (1394), at-Tirmidhiy (2949), ambaye amesema kuwa ni nzuri na Swahiyh, Ibn Maajah (1347). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (1394).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 41
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/33-bora-katika-kisomo-cha-qur-aan/