Inampasa kudumisha kusoma Qur-aan na kuzidisha kusoma kwake. Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa na ada tofauti katika kiwango cha kuisoma Qur-aan yote. Ibn Abiy Daawuud amepokea kutoka kwa baadhi ya Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba walikuwa wanaisoma Qur-aan yote mara moja katika kila miezi miwili, wengine katika kila mwezi wanaisoma yote mara moja, wengine wanaisoma yote katika kila siku kumi mara moja, wengine wanaisoma yote katika kila siku nane, wengi wao wanaisoma yote katika kila siku saba, wengine wanaisoma yote katika kila siku sita, wengine wanaisoma yote katika kila siku tano, wengine wanaisoma yote katika kila siku nne, wengine wanaisoma yote katika kila siku tatu, wengine wanaisoma yote katika kila siku mbili, baadhi ya wengine walikuwa wanaisoma yote kila mchana na usiku, miongoni mwao walikuwa wanaisoma yote mara mbili kila mchana na usiku, miongoni mwao walikuwa wanakamilisha mara tatu, baadhi ya wengine wakiisoma yote mara nane; mara nne usiku na nne mchana.
Miongoni mwa waliokuwa wakikamilisha mara moja kila mchana na usiku ni ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh), Tamiym ad-Daariy, Sa´iyd bin Jubayr, Mujaahid na ash-Shaafi´iy.
Miongoni mwa waliokuwa wakikamilisha mara tatu ni Sulaym bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh), qaadhi wa Misri katika zama za Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh). Abu Bakr bin Abiy Daawuud amepokea kwamba alikuwa akikamilisha katika usiku mara nne. Abu ´Umar al-Kindiy amepokea katika ”Qudhwaatu Miswr” ya kwamba alikuwa akiisoma yote katika usiku mara nne.
Shaykh na Imaam mwema Abu ´Abdur-Rahmaan as-Sulamiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba amemsikia Shaykh Abu ´Uthmaan al-Maghribiy akisema:
”Ibn-ul-Kaatib alikuwa akiisoma yote mara nne mchana na usiku mara nne.”
Hiki ndio kiwango cha juu tulichokifikia ndani ya mchana na usiku mmoja.
Ahmad ad-Dawraqiy ameeleza kwamba Mansuur bin Zaadhaan, mmoja katika wafanya ´ibaadah wa wanafunzi wa Maswahabah:
”Alikuwa akiisoma Qur-aan yote kati ya Dhuhr na ´Aswr, na pia akiisoma yote kati ya Maghrib na ´Ishaa ndani ya Ramadhaan mpaka ipite robo ya usiku.”
Ibn Abiy Daawuud amepokea kwa cheni ya wapokezi:
”Mujaahid alikuwa akiisoma Qur-aan yote kati ya Maghrib na ´Ishaa ndani ya Ramadhaan.”
Mansuur amesema:
”´Aliy al-Azdiy alikuwa akiisoma Qur-aan yote kati ya Maghrib na ´Ishaa kila usiku wa Ramadhaan.”
Ibraahiym bin Sa´d amesema:
”Baba yangu alikuwa anakaa kwa kukumbatia magoti yake na hakuwa anafungua kukaa kwake mpaka aimalize Qur-aan yote.”
Kuhusu yule anayeisoma Qur-aan yote katika Rak´ah moja, hawawezi kuhesabika kutokana na wingi wao. Miongoni mwa waliotangulia ni ´Uthmaan bin ´Affaan, Tamiym ad-Daariy na Sa´iyd bin Jubayr, ambao walikuwa wanaisoma yote katika kila Rak´ah kwenye Ka´bah.
Ni wengi wale waliokuwa wanaisoma yote mara moja ndani ya wiki. Kitendo hicho kimepokelewa kutoka kwa ´Uthmaan bin ´Affaan, ´Abdullaah bin Mas´uud, Zayd bin Thaabit na Ubayy bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anhum). Kitu kama hicho kimepokelewa kutoka kwa jopo la wanafunzi wa Maswahabah kama ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, ´Alqamah na Ibraahiym (Rahimahumu Allaah).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 40-41
- Imechapishwa: 26/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 40-41
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/32-kisomo-cha-qur-aan-cha-salaf/