35. Tofauti kati ya Tawassul ya shirki na Tawassul ya Bid´ah

Ni juu yetu kutofautisha kati ya hali hizi mbili:

1- Yule mwenye kumuabudu huyo aliyemfanya kuwa mkatikati kwa njia ya kwamba akamchinjia na akamuwekea nadhiri ili kujikurubisha kwake.

2- Yule ambaye hamuabudu. Isipokuwa anamfanya kwa madai ya kwamba eti anamfikishia haja zake kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na jaha yake, wema wake na nafasi yake mbele ya Allaah. Hili ni batili na ni Bid´ah. Kwa sababu ni kuzua kitu katika dini ambacho Allaah hakukiidhinisha. Vilevile ni njia inayopelekea katika shirki.

Wale waliokuja nyuma hawatosheki kuweka tu mkatikati na kutomfanyia kitu katika ´ibaadah. Mara nyingi huwa wanamuabudu, wanamchinjia na wanamuwekea nadhiri, kama wanavyofanya kwenye makaburi, wanatufu kwenye hayo makaburi, wanatabaruku kwa udongo wake, wanahiji kwenye kaburi hilo katika nyakati maalum, wanakaa hapo kwa kipindi kirefu, wanawaleta wanyama wao hapo ambapo wanawachinja kwenye makaburi hayo ambapo wanajikurubisha kwa makaburi hayo na kwa wale waliyomo ndani ya makaburi hayo kwa madai kwamba wanawakurubisha kwa Allaah na kwamba eti wanamfikishia Allaah haja zao. Hii ndio hali yao na kitu wanachokitilia umuhimu tokea hapo kale na tangu wakati kulianzwa kujengwa misikiti juu ya makaburi. Hivo ndivyo alivyokhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yametokea yale aliyoeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 62
  • Imechapishwa: 06/08/2018