Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake asimtukane, asimkejeli au kusema kuwa muonekano wake au matendo yake ni mabaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipotaja haki za mwanamke kwa mume wake:

“… na asimkebehi.”[1]

[1] Abu Daawuud (2142), Ibn Maajah (1850), Ibn Hibbaan (9/2764), al-Haakim (2/2764) na Ahmad (4/446-447). Mnyororo ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy ameafikiana na hilo na hali kadhalika al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2033).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 24/03/2017