Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake ni yeye kutompiga. Hakuruhusiwa kumpiga mke isipokuwa pale atapochelea uasi kutoka kwake na akawa anamuasi mume wake. Kipigo kitatumika baada ya kumpa mawaidha na kumhama na yakawa hayakusaidia kitu. Hapo ndipo mume anaruhusiwa kumpiga. Lakini ampige kwa njia ya kumtia adabu na sio kwa njia kisasi. Haruhusiwi kabisa kumpiga kwenye uso. Ni dhuluma kumpiga mke kwa kitu ambacho hukupewa idhini kwacho na kwa njia ambayo hukupewa idhini kwayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atayepiga kwa dhuluma atakabiliwa na adhabu siku ya Qiyaamah.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema pia wakati alipokuwa anataja haki za mke juu ya mume wake:

“Asimpige usoni.”[2]

Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

“Na wale [wanawake] ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na [wakiendelea uasi] wahameni katika malazi [vitanda] na [mwishowe wakishikilia uasi] wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia [ya kuwaudhi bure]. Hakika Allaah ndiye Aliye juu na Mkuu.”[3]

Wafasiri wa Qur-aan wamesema mwanamke akimtii mume wake hana haki yoyote ya kumpiga wala kumhama. Allaah (Ta´ala) Amesema mwishoni:

إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

“Hakika Allaah ndiye Aliye juu na Mkuu.”

ni tishio kwa waume. Wakiwavamia wake basi wajue kuwa Aliye juu na Mkuu ndiye Mlinzi wao na atawalipia kwa wale wenye kuwadhulumu.

Ukijiona kuwa una manguvu na ni muweza wa kumpiga mke wako bila ya sababu yoyote sahihi kutoka kwa Allaah, basi kumbuka ya kwamba [mwanamke huyo] ana Mlinzi ambaye juu ya kila jambo ni muweza na kuwa Yeye yu juu na ni Mkuu. Ninakuonya kumuudhi Mola Wako. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ama kuhusu haki zenu juu ya wake zenu, wasimwache yeyote mnayemchukia akakaa kwenye vitanda vyenu au kuingia manyumba yenu. Wakifanya hivo, basi wapigeni kipigo kisichoumiza.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwapige waja wa Allaah.” Akaja ´Umar na kusema: “Hivyo wanawake watakuja kuwaasi waume zao.” Baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ni sawa mkiwapiga.”[4]

Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwacha mume kumpiga mke? Kwa sababu wakati alipowakataza kabisa waume kuwapiga wanawake baadhi ya wanawake wakaanza kuwaasi waume zao. Kwa ajili hiyo wakaja wanawake wengi kwa wakeze Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwashtaki waume zao. Hapo ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wanawake wengi wamekuja kwa wakeze Muhammad na wanawashtaki waume zao. Hao sio katika [wanaume] wabora wenu. Hao sio katika [wanaume] wabora wenu.”[5]

Si vizuri kumpiga mke wako kwa yale ambayo Allaah (´Azza wa Jall) Hakukupa idhini kwayo.

[1] al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad” (186) na al-Bazzaar (17/9535). Mnyororo ni mzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (5/467).

[2] Ahmad (4/446-447), Abu Daawuud (2142), Ibn Maajah (1850), Ibn Hibbaan (9/4175) na al-Haakim (2/2764). Mnyororo ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim na adh-Dhahabiy amaeafikiana na hilo na kadhalika al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2033).

[3] 04:34

[4] Abu Daawuud (2146), an-Nasaaiy (5/9167), Ibn Maajah (1985), at-Twabaraaniy (1/270), Ibn Hibbaan (9/4189) na al-Haakim (2/2765) ambaye pia amesema kuwa ni Swahiyh. Tazama ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (6/1863) ya al-Albaaniy.

[5] al-Bukhaariy (5363).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 48-50
  • Imechapishwa: 24/03/2017