Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wapo kamuua mwingine kisha wote wawili wakaingia Peponi.”[1]

MAELEZO

12 – Kucheka. Kucheka ni miongoni mwa sifa za Allaah zilizomthubutikia kwa Sunnah na maafikiano ya Salaf. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wapo kamuua mwingine kisha wote wawili wakaingia Peponi.”

Ukamilifu wa Hadiyth:

“Mmoja anapigana vita katika njia ya Allaah ambapo akakufa kisha Allaah akamsamehe aliyeua na akafa shahidi.”[2]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah kucheka. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kuifanyia namna wala kuipigia mfano. Ni kucheka kikweli ambako kunalingana na Allaah (Ta´ala).

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni thawabu. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne.

[1] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).

[2] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 26/10/2022