35. Hapa ndipo mwanamke anapaswa kuvaa jilbaab

Jengine ni kwamba maneno yake ”Jilbaab wakati wa kutoka”hayana maana ya pili. Kwani mwanamke anatakiwa kuvaa jilbaab mbele ya wanamme ambao ni kando naye ili wasione mapambo yake, ni mamoja ametoka nyumbani au yuko ndani ya nyumba. Kwa maana nyingine ni lazima kwa mwanamke kuvaa jilbaab katika hali zote. Kinachotilia nguvu hayo ni maneno yake Qays bin Zayd:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtaliki Hafswah bint ´Umar… Wakati mmoja akaja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyumbani kwake ambapo akajisitiri. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Hakika Jibriyl amenijia na akasema: ”Mrejee Hafswah. Hakika ni mwanamke mwenye kufunga na mwenye kusimama usiku kuswali na ndiye mke wako Peponi.”[1]

[1] Ibn Sa´d na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kupitia kwa Hammaad bin Salamah ambaye amesimulia kuwa Abu ´Imraan al-Juuniy amemukhabarisha. Wapokezi wake wote ni wenye kuaminika na ni wanamme wa Muslim. Hata hivyo kuna makinzano juu uswahabah wa Qays bin Zayd. Ibn ´Abdil-Barr amesema:

”Inasemekana kuwa Hadiyth zake wanakosekana Maswahabah katika cheni zake na yeye mwenyewe hakuwa Swahabah.”

Haafidhw Ibn Hajar amesema katika ”al-Iswaabah”:

”Mwanafunzi mdogo wa Maswahabah. Amezitaja Hadiyth pasi na Maswahabah kwenye cheni zake za wapokezi. Kuna wengi – akiwemo al-Haarith bin Abiy Usaamah – amemwingiza katika Maswahabah. Ibn Abiy Haatim na wengineo kwa kumfuata al-Bukhaariy wamemwingiza katika wanafunzi wa Maswahabah.”

Hadiyth kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi. al-Haythamiy amesema:

”Ameipokea at-Twabaraaniy na wasimulizi wake ni wasimulizi wa Swahiyh.” (Majma´-uz-Zawaa-id)

al-Haakim pia ameipokea na vilevile akaitajia upokezi mwingine wenye kuitilia nguvu kutoka kwa Anas inayotiwa nguvu kwayo. Hata hivyo humo hakukutajwa jilbaab. Vilevile Ibn Sa´d ameipokea kwa ufupi kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh. Ibn Sa´d ameipokea tena kupitia kwa Habiyb bin Abiy Thaabit:

”Umm Salamah amesema: ”Wakati ilipomalizika eda yangu kwa Abu Salamah, alinijia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyumbani kwangu. Akanizungumzisha baina yangu mimi na yeye kulikuwa pazia na akanichumbia.”

Udhahiri ni kwamba pazia iliyokusudiwa ni ukuta au kizuizi kingine na sio nguo ambayo mwanamke anajisitiri kwayo. Hayo ndio makusudio ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

”Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:53)

Imesihi pia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba alikuwa akivaa jilbaab wakati anaposwali. Kwa hivyo ikajulisha kuwa jilbaab sio maalum wakati wa kutoka nje ya nyumba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 19/09/2023