34. Ujinga wa watu wengi kutoitambua Tawhiyd na shirki

na ukajua jambo lililowapitikia watu wengi kwa kuwa wajinga juu ya hili,

MAELEZO

Kuwa na ujinga juu ya Tawhiyd na shirki. Haya ndio yaliyowapelekea watu wengi katika upotevu. Nako ni kwamba hawaijui Tawhiyd sahihi na hawaijui shirki na kila kimoja katika hivyo wanakifasiri kinyume na tafsiri yake sahihi. Haya ndio yamewafanya watu wengi kutumbukia katika makosa, kufuru, shirki, Bid´ah na mambo ya uzushi. Hayo ni kwa sababu ya kutokujua yale Allaah aliyoamrisha katika kumpwekesha na kumtii na yale Allaah aliyokataza katika shirki na kumuasi. Wasiokuwa wasomi hawajui na wanachuoni wengi wa falsafa wameshughulishwa na elimu ya falsafa na ya mantiki ambayo ndio wamejenga juu yake ´Aqiydah zao. Haifanyi haki kuwa haki na wala haifanyi batili kuwa batili. Mambo ni kama walivyosema baadhi ya wanachuoni:

“Hainufaishi kuitambua na wala haidhuru kutoitambua.”[1]

[1] Tazama ”Radd ´alaa al-Mantwiqiyyiyn”, uk. 03 ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 25/11/2016