Vivyo hivyo inahusiana na Hadiyth ya Kuonekana:
“Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi usiku wa mwezi mng’aro – hamtosongamana katika kumuona.”
Bi maana mtamuona waziwazi kabisa. Kumuona kutakuwa wazi kabisa kiasi cha kwamba haihitajii msongamano. Kitu kisichokuwa wazi pengine watu wakasongamana na kuambizana wakitazame kwa ajili ya kutoonekana kwake vizuri. Ama kuhusiana na Kuonekana Kwake (Subhaanah) kutakuwa waziwazi kabisa kama mfano wa linavyoonekana jua pasi na mawingu. Kutakuwa hakuna haja ya kusongamana, kubanana na rabsha. Kila mmoja atamuona akiwa yuko sehemu yake bila ya kupata usumbufu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 68-69
- Imechapishwa: 24/10/2024
Vivyo hivyo inahusiana na Hadiyth ya Kuonekana:
“Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi usiku wa mwezi mng’aro – hamtosongamana katika kumuona.”
Bi maana mtamuona waziwazi kabisa. Kumuona kutakuwa wazi kabisa kiasi cha kwamba haihitajii msongamano. Kitu kisichokuwa wazi pengine watu wakasongamana na kuambizana wakitazame kwa ajili ya kutoonekana kwake vizuri. Ama kuhusiana na Kuonekana Kwake (Subhaanah) kutakuwa waziwazi kabisa kama mfano wa linavyoonekana jua pasi na mawingu. Kutakuwa hakuna haja ya kusongamana, kubanana na rabsha. Kila mmoja atamuona akiwa yuko sehemu yake bila ya kupata usumbufu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 68-69
Imechapishwa: 24/10/2024
https://firqatunnajia.com/34-sifa-na-majina-ya-allaah-yaliyothibiti-katika-sunnah-iv/