Jengine ni kwamba al-Jahm anadai jambo jengine. Anasema kuwa Allaah (Ta´ala) amesema:

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

”Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake ndani ya siku sita, kisha akalingana juu ya ‘Arshi.”[1]

Akadai kuwa Qur-aan ima iwepo kwenye mbingu, ardhini au katikati ya viwili hivyo. Hivyo akaeneza shubuha kati ya watu na kuwatia mchanga wa machoni. Nikamuuliza kuwa Allaah (´Azza wa Jall) si ameeleza kwamba uumbaji na viumbe ilikuwa kwenye mbingu, ardhi na vilivyomo baina yake, akaitikia ndio. Kisha nikamuuliza kama kuna viumbe vilivyopo juu ya mbingu, wakaitikia ndio. Hata hivyo hakuingiza viumbe juu ya mbingu pamoja na vile vitu vilivyoumbwa. Wanazuoni wamejua juu ya mbingu saba kuna Kursiy, ´Arshiy na Ubao uliohifadhiwa, Pazia na vyengine vingi ambavyo hakuvitaja. Hata hivyo hakuviingiza katika vile vitu vilivyoumbwa. Allaah amezielezea tu mbingu, ardhi na vilivyomo baina yake.

Isitoshe tukakabiliana na madai yao ya kwamba Qur-aan ima iwe ndani ya mbingu, ardhi au vilivyomo baina yake kwa maneno Yake Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ

”Je, hawatafakari katika nafsi zao Allaah hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki?”[2]

Ambacho mbingu na ardhi viliumbwa kwacho kilikuwepo kabla ya mbingu na ardhi. Haki ambayo mbingu na ardhi viliumbwa kwayo ni maneno Yake, kwa sababu Allaah anasema:

قَالَ فَالْحَقُّ وَالْحَقَّ أَقُولُ

”Akasema: ”Basi haki inatoka Kwangu – na haki Naisema.”[3]

وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ

”… na Siku atakaposema: ”Kuwa!” basi huwa. Na maneno Yake ni haki.”[4]

Haki ambayo mbingu na ardhi zimeumbwa kwayo ilikuwepo kabla  ya mbingu na ardhi. Haki ni yale maneno Yake – na maneno Yake hayakuumbwa[5].

[1] 32:4

[2] 30:8

[3] 38:84

[4] 06:73

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 24/04/2024