34. Mazuri na mabaya, kheri na shari yameshakadiriwa

Ahl-us-Sunnah wanashuhudia na kuitakidi ya kwamba kheri na shari, manufaa na madhara, yanatokea kwa mipango na makadirio ya Allaah. Hakuna njia ya kuyarudisha, kuyaepuka wala kuyakwepa. Hakuna kinachompata mtu isipokuwa kile alichomwandikia Mola Wake. Endapo viumbe wote watakusanyika kwa ajili ya kumnufaisha mtu kwa kitu ambacho Allaah hajamwandikia, basi hawatoweza kumnufaisha. Na endapo viumbe wote watakusanyika kwa ajili ya kumdhuru mtu kwa kitu ambacho Allaah hajamwandikia, basi hawatoweza  kumdhuru, jambo ambalo ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amelisimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ

”Allaah akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye, na akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhilah Zake.”[1]

[1] 10:107

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 284
  • Imechapishwa: 20/12/2023