34. Matahadharisho ya kuchupa mipaka katika kusoma sarufi

150 – Abu Nu´aym al-Haafidhw ametukhabarisha: Abu Bakr Muhammad bin al-Fath al-Hanbaliy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Abiy Daawuud ametuhadithia: Kathiyr bin ´Ubayd ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Abiy Hawshab: Nimemsikia al-Qaasim bin Mukhaymirah akisema:

”Kujifunza sarufi kunaanza kwa kujishughulisha na kumalizikia kwa kuvuka mipaka.”

151 – ´Abdullaah bin ´Umar bin Ahmad al-Waa-idhw ametukhabarisha: Baba yangu ametuhadithia: Muhammad bin al-´Abbaas bin Shujaa´ ametuhadithia: Ayyuub bin Sulaymaan ametuhadithia: ´Abdul-Hamiyd bin Ibraahiym Abu Tuqaa ametuhadithia: Salamah bin Kulthuum ametuhadithia: Nimemsikia Ibraahiym bin Ad-ham, kutoka kwa Maalik bin Diynaar, aliyesema:

”Unaweza kukutana na mtu asiyefanya kosa hata moja katika utamkaji ilihali matendo yake yote ni makosa matupu ya utamkaji.”

152 – Abul-Qaasim al-Azhariy amenihadithia: Muhammad bin al-´Abbaas al-Kharraaz ametuhadithia: Ibn Abiy Daawuud ametuhadithia: ´Abdullaah bin Khubayq ametuhadithia: Nimemsikia Shaykh mmoja kutokea Dameski akisema: Ibraahiym bin Ad-ham amesema:

”Tunatamka kisarufi na hivyo hatufanyi makosa katika utamkaji, lakini tunafanya utamkaji wa makosa katika matendo na hivyo hatuzungumzi sarufi kwa kupatia.”

153 – Abul-Hasan ´Aliy bin Ayyuub al-Qummiy amenikhabarisha: Abu ´Ubaydillaah Muhammad bin ´Imraan al-Marzubaaniy ametuzindua: as-Swuuliy amenikhabarisha: Bwana mmoja anayeipa nyongo dunia amesema:

Hatukusibiwa kutokana na ujinga

lakini tunaificha elimu kwa ujinga

Tunachukia kufanya makosa katika utamkaji wetu

na tunapuuza kufanya makosa katika utendaji wetu

154 – ´Abdullaah bin ´Umar bin Ahmad al-Waa´idhw ametukhabarisha: Baba yangu ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad ametuhadithia: Naswr bin ´Aliy al-Jahdhwamiy ametuhadithia: Muhammad bin Khaalid amenihadithia: ´Aliy bin Naswr – yaani baba yake – amenihadithia:

”Nilimuota al-Khaliyl bin Ahmad usingizini nikasema: ”Simuoni mtu mwenye akili zaidi kumshinda al-Khaliyl.” Nikasema: ”Allaah amefanya nini na wewe?” Akasema: ”Unajua yale yote tuliyokuwemo? Hakika sijaona kitu kilicho bora kama:

سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ

”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, himdi zote njema ni za Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni mkubwa.”

155 – Abu Bakr Ahmad bin al-Mubaarak bin Ahmad al-Baraathiy ametukhabarisha: ´Aliy bin Muhammad bin Muusa at-Tammaar ametuhadithia huko Baswrah: Abu ´Iysaa Jubayr bin Muhammad ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdillaah at-Tirmidhiy ametuhadithia: Nimemsikia Naswr bin ´Aliy akisema: Nimemsikia baba yangu akisema:

”Nilimuota al-Khaliyl bin Ahmad usingizini nikasema: ”Amekufanya nini Mola wako?” Akasema: ”Amenisamehe.” Nikasema: ”Umesalimika kwa kitu gani?” Akasema: ”Kwa:

لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ الْعَلِيِّ الْعَظِيمِ

”Hapana hila wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Aliye juu kabisa, Aliyetukuka.”

Nikasema: ”Umeikuta vipi elimu yako?” Bi maana metriki, fasihi na mashairi. Akajibu: ”Nimekuta si lolote si chochote.”

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 89-91
  • Imechapishwa: 22/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy