Swali: Je, inasihi kuswali nyuma ya anayemwomba uokozi asiyekuwa Allaah na anatamka mfano wa maneno haya:

“Niokoe na nisaidie ee Jaylaaniy.”

Ikiwa sikumpata mwengine inafaa kwangu kuswali nyumbani kwangu?

Jibu: Haijuzu kuswali nyuma ya washirikina wote kukiwemo yule anayeomba uokozi na msaada kutoka kwa asiyekuwa Allaah. Kwa sababu kuomba uokozi kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika wafu, masanamu, majini na viumbe venginevyo ni kumshirikisha Allaah (Subhaanah). Ama kuwaomba uokozi viumbe waliohai, walio mbele yako na wanaoweza kukusaidia ni sawa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema katika kisa cha Muusa:

فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

“Akamsaidia yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake.”[1]

Usipompata imamu muislamu unayeweza kuswali nyuma yake itafaa kwako kuswali nyumbani kwako. Ukipata kikosi cha watu waislamu ambao wanaweza kuswali msikitini kabla au baada ya yule imamu mshirikina, basi mswali pamoja nao. Waislamu wakiweza kumng´oa imamu huyo mshirikina na kumteua imamu muislamu ambaye anaweza kuwaswalisha watu basi itawalazimu kwao kufanya hivo. Kwa sababu kufanya hivo ni katika kuamrisha mema na kukemea maovu na kusimamisha Shari´ah ya Allaah ardhini ikiyumninika kufanya hivo pasi na mtihani. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[2]

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote katika nyinyi atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake, asipoweza basi afanye hivo kwa mdomo wake, asipoweza basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu mno.”[4]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] 28:15

[2] 09:71

[3] 64:16

[4] Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 121-122
  • Imechapishwa: 19/07/2022