Kupenda (الولاية) na kujitenga mbali (البراءة) ni Bid´ah. Nao ni wale wanaosema kuwa wanawapenda baadhi na wanajitenga mbali na wengine. ´Aqiydah hii ni Bid´ah, tahadhari nayo[1].
Yule atakayesema chochote katika Bid´ah hizi, akazionelea, akazitamani, akaziridhia au akazipenda, basi ameenda kinyume na Sunnah, ametoka nje ya Mkusanyiko, ameacha mapokezi, ameonelea kinyume, ameingia ndani ya Bid´ah na amepinda kutokamana na njia.
Tawfiyq yetu iko kwa Allaah. Kwake ndio twategemea na tunataka msaada Kwake na hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.
[1] Abu Twaalib amesema:
”Nilimuuliza Abu ´Abdillaah kama kujitenga mbali, kupenda na kushuhudia ni Bid´ah. Akajibu: ”Kujitenga mbali inahusiana na kujitenga mbali na mmoja katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kupenda inahusiana na kuonyesha mapenzi kwa baadhi mbali na wengine. Kuhushudia inahusiana na kukata kuwa mmoja wao yuko Motoni.” (al-Khallaal (763))
- Muhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 95-96
- Imechapishwa: 08/06/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)