Vinginevyo kulingania kwa Allaah kutakuwa na maana gani? Tunawalingania katika ukweli, kutofanya ghushi katika biashara, kuacha ribaa, uzinzi na tunaacha shirki na hatuwalinganii watu kuiacha? Tunaacha khatari kubwa? Ni wajibu tuanze na Tawhiyd na kukataza shirki. Kuhusu madhambi mengine yako chini ya matakwa ya Allaah. Lakini shirki Allaah hakubali msamaha na wala haiingi chini ya matakwa ya msamaha wa Allaah. Vipi tutaanza na kushikamana na mataga na mambo madogomadogo na tukaacha mambo? Huku sio kulingania katika dini ya Allaah.
Mitume kitu cha kwanza walianza nacho ni kuzisahihisha ´Aqiydah na kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Hawakuanza kwa mambo yasiyofaa pamoja na kukosekana Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi.
Lau ikiwa mtu ataacha zinaa, kunywa pombe, ribaa na mambo mengine yote ya haramu isipokuwa tu akawa ni mshirikina, yote hayo hayatomfaa kitu hata ijapokuwa atakuwa ni mwenye kuswali usiku na mchana, anatoa swadaqah kwa mali yake yote maadamu ana shirki kubwa hayatomfaa kitu. Lakini kinyume chake, lau atakuwa na Tawhiyd anamtakasia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall) na akasalimika na shirki, ijapokuwa atakuwa ni mwenye kufanya baadhi ya madhambi makubwa, kunatarajiwa juu yake msamaha. Na ikiwa ataadhibiwa hakika hatodumishwa milele katika adhabu. Vipi tunaacha jambo la khatari na tunalipa umuhimu lililo chini yake na tunasema huku ndio kulingania katika dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Leo mnajua juhudi za kulingania kwa Allaah. Walinganizi wanaolingania katika dini ya Allaah, taasisi na vituo vimekuwa vingi. Lakini makaburi bado yako palepale na bali yanaongezeka katika ulimwengu wa Kiislamu. Taswawwuf na Bid´ah vimeenea. Kuko wapi kulingania kwa Allaah? Juhudi hizi na matunda yako wapi?
Ni wajibu juu yetu kuzinduka na jambo hili, tulinganie katika dini ya Allaah kwa ujuzi na tuanze kwa walichoanza nacho Manabii na Mitume ambacho ni kuzisahihisha ´Aqiydah. Kisha baada ya hapo ndio kujenga juu yake. Kwa sababu ndio msingi na mengineyo yanajengwa juu yake. Msingi ukiwa sahihi na nyumba itakuwa sahihi. Msingi ukiwa mbovu basi nyumba itaanguka wala haitomfaa mwenye nayo:
أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
”Je, yule ambaye ameasisi jengo lake katika taqwa ya Allaah na radhi ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa lenye kuburugunyika likaporomoka pamoja naye katika moto wa Jahannam? Allaah haongoi watu madhalimu.”(at-Tawbah 09:109)
Huu ni mfano ulio wazi kwa yule aliyeijenga dini yake juu ya ´Aqiydah sahihi na nia njema na yule aliyeijenga dini yake juu ya shirki na juu ya mambo mengine yanayokwenda kinyume na dini ya Allaah. Huu ni mfano wa wazi katika Qur-aan tukufu.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 54-56
- Imechapishwa: 06/08/2018

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 54-56
Imechapishwa: 06/08/2018
https://firqatunnajia.com/33-uwajibu-wa-kuanza-kulingania-katika-tawhiyd-kabla-ya-kila-kitu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)