Ikiwa mwanamke atakuwa anaswali mbele ya wanaume wasiokuwa maharimu, basi afunike uso wake. Imekuja katika ”al-Mughniy” (2/331):

“Ibn ´Abdil-Barr amesema: ”Hakika wanazuoni wameafikiana juu ya kwamba ni wajibu kwa mwanamke kufunua uso wake katika swalah na ndani ya Ihraam.”

Kuishia kufunua uso tu ndani ya swalah – kitu ambacho wanazuoni wameafikiana – ndicho kilicho bora zaidi na kilicho na tahadhari zaidi.

Ama kuhusu kijakazi akiswali huku kichwa chake kikiwa wazi, basi swalah yake ni sahihi kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, isipokuwa al-Hasan, kama ilivyonukuliwa katika ”al-Mughniy (2/331). Wanazuoni wametofautinaa kuhusu kufunua sehemu nyingine zisizokuwa kichwa. Lililo bora kwa kijakazi ni kuwa kama mwanamke muungwana katika aibu ya kujisitiri na kuwa na aibu ndani ya swalah na nje yake.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 27/05/2026