Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Sharti ya saba ni kuingia kwa wakati. Dalili ya hilo ni kutoka katika Sunnah kwenye Hadiyth ya Jibriyl (´alayhis-Salaam) alipomswalisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanzoni mwa wakati wa swalah na mwishoni wa wakati wake. Akasema:
“Ewe Muhammad! Swalah ni baina ya nyakati hizi mbili.”[1]
Kadhalika Amesema (Ta´ala):
إِنَّ الصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
“Hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekewa nyakati maalumu.”[2]
Bi maana imefaradhishwa kwa wakati wake. Dalili ya kuingia kwa wakati wake ni Kauli Yake (Ta´ala):
أَقِمِ الصَّلاَةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا
“Simamisha swalah pale jua linapoanza kupinduka mpaka kiza cha usiku na swalah ya alfajiri; hakika swalah ya alfajiri ni yenye kushuhudiwa.”[3]
MAELEZO
Miongoni mwa masharti ya kusihi kwa swalah ni kutekeleza swalah tano ndani ya nyakati zake. Kwa msemo mwingine ni kwamba haijuzu kuziswali kabla ya wakati wake. Ikitokea mtu ameswali kabla ya wakati wake basi ni lazima azirudie. Haijuzu pia kuichelewesha swalah hadi ukapita wakati wake. Ikiwa ataichelewesha mpaka uaktoka wakati wake, ikiwa ni kwa sababu ya usingizi ambao haukuwa kwa uzembe au kwa sababu ya kusahau, basi atailipa bila dhambi juu yake. Lakini ikiwa ataichelewesha bila udhuru huo basi amefanya dhambi, na analazimika kuilipa. Hadiyth ya Jibriyl kumswalisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya siku mbili imepokewa kutoka kwa kundi la Maswahabah, miongoni mwao ni Ibn ´Abbaas na Jaabir. Ipo kwa Abu Daawuud (393–394) na at-Tirmidhiy (149–150). Angalia pia maelezo ya Hadiyth hiyo (3081) na Hadiyth (11249) katika ”Musnad” ya Imaam Ahmad.
Miongoni mwa yaliyobainisha wazi kuhusu nyakati za swalah tano ni Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) katika ”as-Swahiyh” ya Muslim (612) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wakati wa Dhuhr ni pale jua linapopinda kutoka katika kilele chake na kivuli cha mtu kiwe mfano wa urefu wake mradi tu ´Aswr haijaingia. Wakati wa ´Aswr ni mpaka jua lianze kuwa na rangi ya manjano. Wakati wa Maghrib ni mpaka mwanga wa machweo utoweke. Wakati wa ´Ishaa ni hadi nusu ya usiku wa kati. Wakati wa Subh ni kuanzia kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuchomoza kwa jua. Ikiwa jua litaanza kuchomoza basi jizuie kuswali, kwa sababu huchomoza kati ya pembe mbili za shaytwaan.”
[1] Abu Daawuud (393) na tamko ni lake, at-Tirmidhiy (149), Ahmad (3081), Ibn Khuzaymah (325), al-Haakim (17193) na wengineo. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (377).
[2] 04:103
[3] 17:78
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 38-39
- Imechapishwa: 27/05/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 38-39
Imechapishwa: 27/05/2026
https://firqatunnajia.com/34-sharti-ya-saba-ya-swalah-ni-kuinga-wakati-wa-swalah/