Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Sharti ya nane ni kuelekea Qiblah. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاء فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوِهَكُمْ شَطْرَهُ
“Hakika Tumeona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni, basi Tutakuelekeza Qiblah kinachokuridhisha. Hivyo basi uelekeze uso wako upande wa Msikiti mtakatifu; na popote mtakapokuwepo basi zielekezeni nyuso zenu upande wake.”[1]
MAELEZO
Ni sharti katika utekelezaji wa swalah iwe ni kuelekea upande wa Qiblah, nayo ni Ka´bah Tukufu. Ikiwa mtu yupo mjini au karibu na watu wanaojua upande wa Qiblah, basi ni lazima aulize upande gani kipo. Haijuzu kwake kuswali kwa kujitahidi ilihali kuna mtu wa kumuelekeza. Ikiwa ataswali kisha akagundua kwamba ameswali kinyume na Qiblah, basi ni lazima arudie swalah. Lakini akiwa safarini, basi anajitahidi kutambua upande wa Qiblah. Akiwa ameswali na baadaye ikabainika kwamba ameswali kinyume na Qiblah, basi swalah yake ni sahihi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[2]
[1] 02:144
[2] 64:16
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 39-41
- Imechapishwa: 27/05/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Sharti ya nane ni kuelekea Qiblah. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاء فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوِهَكُمْ شَطْرَهُ
“Hakika Tumeona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni, basi Tutakuelekeza Qiblah kinachokuridhisha. Hivyo basi uelekeze uso wako upande wa Msikiti mtakatifu; na popote mtakapokuwepo basi zielekezeni nyuso zenu upande wake.”[1]
MAELEZO
Ni sharti katika utekelezaji wa swalah iwe ni kuelekea upande wa Qiblah, nayo ni Ka´bah Tukufu. Ikiwa mtu yupo mjini au karibu na watu wanaojua upande wa Qiblah, basi ni lazima aulize upande gani kipo. Haijuzu kwake kuswali kwa kujitahidi ilihali kuna mtu wa kumuelekeza. Ikiwa ataswali kisha akagundua kwamba ameswali kinyume na Qiblah, basi ni lazima arudie swalah. Lakini akiwa safarini, basi anajitahidi kutambua upande wa Qiblah. Akiwa ameswali na baadaye ikabainika kwamba ameswali kinyume na Qiblah, basi swalah yake ni sahihi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[2]
[1] 02:144
[2] 64:16
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 39-41
Imechapishwa: 27/05/2026
https://firqatunnajia.com/35-sharti-ya-nane-ya-swalah-ni-kuelekea-qiblah/