Swali 16: Je, inapendekezwa kufanya Istikhaarah katika Hajj? Ni mambo gani ambayo inapendekezwa ndani yake kufanya Istikhaarah?
Jibu: Istikhaarah imesharifiwa katika kila jambo ambalo mtu anasitasita ndani yake. Kwa mfano ikiwa anasitasita, je, ahiji mwaka huu au asihiji? Basi anaweza kufanya Istikhaarah. Ikiwa tutasema kwamba Hajj si wajibu wa haraka. Ama ikiwa tutasema kwamba ni wajibu wa haraka, basi ni wajibu juu yake ahiji bila kufanya Istikhaarah.
Vilevile kuna mambo ambayo hayahitaji Istikhaarah, kama vile ikiwa mtu amekusudia kuswali au ametaka kula chakula, basi hatoswali swalah ya Istikhaarah. Hakika Istikhaarah huwa pale ambapo mtu yuko katika kusitasita. Kwa sababu hiyo anasema katika du´aa ya Istikhaarah:
”Ee Allaah! Ikiwa Unajua kwamba jambo hili ni kheri kwangu, basi nipangie nalo na unirahisishie nalo.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/26)
- Imechapishwa: 27/05/2026
Swali 16: Je, inapendekezwa kufanya Istikhaarah katika Hajj? Ni mambo gani ambayo inapendekezwa ndani yake kufanya Istikhaarah?
Jibu: Istikhaarah imesharifiwa katika kila jambo ambalo mtu anasitasita ndani yake. Kwa mfano ikiwa anasitasita, je, ahiji mwaka huu au asihiji? Basi anaweza kufanya Istikhaarah. Ikiwa tutasema kwamba Hajj si wajibu wa haraka. Ama ikiwa tutasema kwamba ni wajibu wa haraka, basi ni wajibu juu yake ahiji bila kufanya Istikhaarah.
Vilevile kuna mambo ambayo hayahitaji Istikhaarah, kama vile ikiwa mtu amekusudia kuswali au ametaka kula chakula, basi hatoswali swalah ya Istikhaarah. Hakika Istikhaarah huwa pale ambapo mtu yuko katika kusitasita. Kwa sababu hiyo anasema katika du´aa ya Istikhaarah:
”Ee Allaah! Ikiwa Unajua kwamba jambo hili ni kheri kwangu, basi nipangie nalo na unirahisishie nalo.”
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/26)
Imechapishwa: 27/05/2026
https://firqatunnajia.com/istikhaarah-katika-hajj/