Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Inatakiwa kuamini kuwa ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) atashuka na kumuua karibu na mlango wa Ludd.”

MAELEZO

Ludd ipo Shaam. Atauawa na ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) kisha atawahukumu watu kwa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadaye ataoa na kufa ambapo ataswaliwa na waumini wataokuwa katika wakati huo.

Kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ni kwamba alipandishwa juu mbinguni akiwa hai. Dalili ya hilo ni maneno ya (Ta´ala):

وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Wala hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Hakika wale waliotofautiana juu yake wamo katika shaka kutokamana nalo – hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Kwa yakini hawakumuua. Bali Allaah alimnyanyua Kwake. Allaah daima ni Mwenye nguvu zisizoshindika, Mwenye hekima.”[1]

Halafu atashuka chini ardhini na kuhukumu kwa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si kitu kingine. Kwa sababu Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio yenye kuhukumu, ujumbe wake ndio wa mwisho na hakuna Mtume mwingine baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا

“Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Allaah daima ni mjuzi wa kila jambo.”[2]

Wakati utapofika wakati wa ´Iysaa (´alayhis-Salaam) atafariki.

Kinacholengwa ni kwamba miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuamini kujitokeza kwa ad-Dajjaal. Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu wamepinga kujitokeza kwake pasi na elimu na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamethibitisha kwa elimu.

[1] 04:157-158

[2] 33:40

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 17/10/2019