224 – Muhammad bin ´Uthmaan al-´Uqayliy amenihadithia: Muhammad bin Raashid adh-Dhwariyr al-Minqariy ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Umar, kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Hurayrah, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wenye kiburi na madhalimu watakusanywa siku ya Qiyaamah katika sura za chungu. Matokeo yake watu watawakanyaga kutokana na udhalili wao mbele ya Allaah (´Azza wa Jall).”
225 – Ahmad bin Maniy´ na Abu Khaythamah wametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa Azhar bin Sinaan al-Qurashiy, kutoka kwa Muhammad bin Waasiy´ al-Azdiy, ambaye ameeleza: Nilifika kwa Bilaal bin Abiy Burdah na akamwambia: Ee Bilaal! Baba yangu ametuhadithia kwamba baba yake amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Hakika katika Jahannam kuna bonde linaloitwa Habhab. Allaah (´Azza wa Jall) amejifaradhishia ya kwamba atamuweka humo kila mwenye kiburi. Basi jihadhari, ee Bilaal, usiwe miongoni mwa watakao kaa humo!”[1]
226 – Nimehadithiwa kutoka kwa Abu Hammaam: Ibn Wahb ametuhadithia: Ibraahiym bin Nashiytw amenikhabarisha, kutoka kwa ´Umar (mtumwa wa Ghufrah aliyeachwa huru), kutoka kwa Muhammad bin Husayn bin ´Aliy, ambaye amesema:
”Haijaingia katika moyo wa mtu chochote cha kiburi isipokuwa imepunguza akili yake kwa kadiri ya kiwango kilichoingia, kiwe kidogo au kikubwa.”
227 – ´Aliy bin Naswr bin Bujayr amenihadithia, kutoka kwa mzee mmoja kutoka Quraysh, aliyeeleza kwamba al-Hasan amesema:
”Kusujudu huondoa kiburi, na upwekeshaji unaondoa kujionyesha.”
228 – Ibraahiym bin Sa´d amenihadithia: Husayn bin Muhammad ametuhadithia: Ibn Abiy Dhi’b ametuhadithia, kutoka kwa al-Qaasim, kutoka kwa Ibn ´Ayyaash, kutoka kwa Naafiy´ bin Jubayr, ambaye amesema:
”Hakika watu wanasema: ”Yuko na majivuno.” Naapa kwa Allaah! Hakika mimi nimepanda punda na nimevaa joho la sufu.”
229 – Muhammad bin Ja´far amenihadithia: Mansuur ametuhadithia, kutoka kwa ´Ammaar: ´Abdullaah bin Lahiy´ah ametuhadithia, kutok kwa ´Abdullaah bin Hubayrah, ambaye amesema:
”Salmaan aliulizwa kuhusu dhambi ambayo hakuna wema unaofaa pamoja nao, akasema: ”Kiburi.”
230 – Abu Muhammad ametuhadithia: Ibraahiym bin Ziyaad ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, ambaye ameeleza:
”Kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah, hakika fulani ni mwenye majivuno ndani ya nafsi yake!” Akasema: ”Je, si baada yake kuna mauti?”
231 – Bishr bin Mu´aadh al-´Aqadiy amenihadithia: Muhammad bin ´Abdillaah al-Qurashiy amenihadithia: Baba yangu amenihadithia: Yuunus bin ´Ubayd amesema:
”Hakuna kiburi pamoja na kusujudu, na hakuna unafiki pamoja na upwekeshaji.”
[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1743).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 270-275
- Imechapishwa: 30/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 270-275
Imechapishwa: 30/03/2026
https://firqatunnajia.com/33-jambo-linaloondoa-kiburi/