101 – Mutwarrif bin ´Abdillaah bin ash-Shukhayr (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amemsimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika Rukuu´ na Sujuud yake:
سُبُّوُحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ
“Mwingi wa kutakaswa, mtakatifu, Mola wa Malaika na roho [Jibriyl].”[1][2]
Ameipokea Muslim.
102 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika Rukuu´ na Sujuud yake:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي
“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah Mola wetu, na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe.”[3][4]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
103 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaporukuu husema:
اللَّهُمَّ لَكَ رَكَعْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، خَشَعَ لَكَ سَمْعِي، وَبَصَرِي، وَمُخِّي، وَعَظْمِي، وَعَصَبِي
“Ee Allaah! Kwako nimerukuu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, uoni wangu, ubongo wangu, mfupa wangu na hisia zangu.”
Na anaposujudu husema:
اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، سَجَدَ وَجْهِيَ لِلَّذِي خَلَقَهُ، وَصَوَّرَهُ، وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ، تَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسنُ الْخَالِقينَ
“Ee Allaah! Kwako nimesujudu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, uso wangu umemsujudia Yule ambaye kauumba, akautia sura na akapasua usikizi wake na uoni wake. ametakasika Allaah, mbora wa waumbaji.”[5][6]
Ameipokea Muslim.
104 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia: “Nilimkosa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) usiku kitandani. Nikapapasa kumtafuta na mkono wangu ukagusa tumbo la nyayo zake mbili zikiwa zimesimamishwa na yeye yuko katika Sujuud. Alikuwa akisema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ، لاَ أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ، أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ
“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokamana na ghadhabu Zako, kwa msamaha Wako kutokamana na adhabu Yako, naomba hifadhi Kwako, mimi siwezi kukusifu ustahikivo – Wewe ni kama Ulivyojisifu juu ya nafsi Yako.”[7]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna fadhilah za du´aa hii, utukufu wake na kuwekwa kwake katika Shari´ah. Maana yake ni kwamba naomba kinga kwa sifa ya ridhaa kutokana na sifa ya hasira, najilinda kwa kitendo cha kusamehe kutokana na kitendo cha adhabu na najilinda kwa Allaah kutokana na Allaah. Hakuna yeyote ambaye mtu anamuomba ulinzi kwake isipokuwa Allaah pekee. Haifai kuomba kinga kwa chochote kinachotoka nje ya matakwa na uwezo wa Allaah.
[1] Muslim (487).
[2] Imekwishatangulia maana yake katika Hadiyth (92).
[3] al-Bukhaariy (794) na Muslim (484).
[4] Imekwishatangulia maana yake katika Hadiyth (93).
[5] Muslim (771).
[6] Imekwishatangulia maana yake katika Hadiyth (94).
[7] Muslim (486).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 103
- Imechapishwa: 04/11/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 103
Imechapishwa: 04/11/2025
https://firqatunnajia.com/33-duaa-ya-kwenye-sujuud/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket