Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
28- Ameshahukumu muda wao wa kuishi.
MAELEZO
Viumbe wana muda wao wa kuishi na wana mwisho wao. Amesema (Subhaanah):
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
“Kila aliyekuwa juu yake [ardhi] ni mwenye kutoweka na utabakia uso wa Mola wako wenye utukufu na ukarimu.”[1]
كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ
“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa uso Wake.”[2]
Kila chenye kuishi kina muda wake maalum uliopangiwa. Allaah amekwishaukadiria, ima ukawa mrefu au ukawa mfupi. Amesema (Subhaanah):
وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ
“Mwanamke yeyote habebi mimba na wala hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake na hapewi umri mrefu yeyote yule mwenye umri mrefu na wala hapunguziwi katika umri wake isipokuwa yamo kitabuni. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[3]
Muda wa kuishi uko mikononi Mwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ni dalili inayofahamisha juu ya ukamilifu wa uola na uwezo Wake. Anachokitaka huwa na asichokitaka hakiwi.
[1] 55:26-27
[2] 28:88
[3] 35:11
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 48-49
- Imechapishwa: 25/09/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)